Jan 3, 2014

Ulimmiss Black Rhino kwenye hip hop? Asema mwaka huu atairudisha ladha ya hip hop

Ulimmiss Black Rhino kwenye hip hop? Asema mwaka huu atairudisha ladha ya hip hop

Mwaka 2013 tumeona baadhi ya wasanii wa hip hop wakihama na kufanya ngoma kadhaa za miondoko mingine kwa madai ya kulifuata soko, sasa Black Rhino mwaka 2014 soko linaweza kumfuata yeye kwenye hip hop.

Mkali huyo aliyewahi kutisha miaka flani na wimbo wa hip hop ‘Mistari’ ambaye mwaka jana alifanya commercial rap ya wimbo wake ‘Mke Mwema’ amesema mwaka huu amepanga kuirudisha tena ladha ya hip hop kwa kuwa fans wake wameimiss kwa kipindi kirefu.

“2014 kidogo it’s different, kwa sababu mwaka 2014 nahisi najisikia kufanya vitu ambavyo vitakuwa vya hip hop kwa sababu nafikiri kuna vitu ambavyo watu wamevimiss.” Black Rhino ameiambia tovuti ya Times Fm.
Amesema mwaka jana aliamua kufanya aina nyingine ya muziki kwa sababu watu wengi walikuwa wamezoea kumsikia Black Rhino ambaye anafanya crank na michano ya hatari hivyo akaamua kudilika kidogo.

Lakini kwa mwaka huu anairudi tena na hip hop, “kwa hiyo kwa mwaka huu siwezi kufanya nilichofanya kwa mwaka jana, mwaka huu kwa sababu watu walikuwa wamenimiss kwenye hip hop, I think I will get back to hip hop.”

Black Chatter amesema ingawa inaonekana kama nyimbo za kiafrika zinafanya vizuri zaidi kwa Afrika, mtu anaweza kufanya hip hop yenye mahadhi ya kiafrika.

“Ingawa inafahamika kwamba Kwaito zinafanya vizuri sasa hivi na nyimbo za Kinajeria zinabamba zaidi kwa Afrika..hiyo ni kwa Afrika, lakini kama mtu unataka kwenda international inabidi ufanye hip hop. Na kama unafanya hip hop katika level hiyo unayosema uende international na Afrika watu wanapenda sana African flavor kama hizo za kinaijeria, basi unaweza kufanya hip hop ambayo ina mahadhi ya kiafrika. Ni vitu ambavyo vinawezekana.”

chanzo timesfm

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA