Jan 9, 2014

YANGA HIYOOO UTURUKI



















Kikosi cha Young Africans kilipokuwa katika kambi ya mafunzo nchini Uturuki mwaka jana

Msafara wa watu 33 wakiwemo wachezaji 27 unatarajia kuondoka usiku wa leo kuelekea nchini Uturuki kwa shirika la ndege la Uturki (Turkish Airlines) kuweka kambi ya mafunzo kwa muda wa takribani wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya kimataifa.

Kikosi cha Young Africans kitafikia katika Hoteli ya kitalii Sueno Beach Side iliyopo km 70 kutoka katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Antalya ikiwa katika eneo la ufukwe na mji wa kihistoria Magnavat. 

Hii inakua ni mara ya pili mfululizo kwa timu ya Young Africans kwenda kuweka kambi katika jiji la Antalya ambapo msimu uliopita pia iliweza kuweka kambi katika mji huo, kambi ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa baada ya kurejea nchini kwani timu iliweza kucheza mzunguko wa pili pasipo kupoteza mchezo hata mmoja mpaka ilipotwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Timu itaondoka chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa na kocha wa makipa Juma Pondamali amabao wataendelea na mafunzo nchini Uturuki wakati uongozi unaendelea na mchakato wa kumpata kocha mkuu ambaye ataungana na kikosi hicho.

Mkuu wa msafara atakua ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salim Rupia ambaye ataongozana na msafara huo kwa kipindi chote cha wiki mbili mpaka kikosi kitakporejea nchini Januari 23 mwaka huu tayari kwa kmzunguko wa pili. 

Msafara kamili ni kama ifuatavyo:
1. Salim Rupia - Mkuu wa Msafara
2. Baraka Kizuguto - Afisa Habari
3. Charles Mkwasa - Kocha msaidizi
4. Juma Pondamali - Kocha wa Makipa
5. Dr. Suphian Juma - Daktari wa timu
6. Hafidh Salehe - Meneja wa timu

Walinda Mlango : Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi: Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Ibrahim Job na Rajab Zahir

Viungo: Frank Domayo, Hasssan Dilunga, Haruna Niyonzima, Nizar Kahlfani, Hamis Thabit na Bakari Msoud

Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Emmanuel Okwi, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Shaban Kondo na Reliants Lusajo

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA