SAMIA SULUHU AMEPOTOKA! ( CUF )
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)
Office of the Secretary General
Party Headquarters,
P.O. Box 3637 , Zanzibar, Tanzania
6/3/2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Chama Cha Wananchi CUF kimeshangazwa na kusikitishwa na kauli
iliyotolewa na Waziri wa Nchi afisi ya Rais anaeshughulikia mambo ya
Muungano Samia Suluhu Hassan, wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya
habari na kuripotiwa na gazeti la Serikali Daily News la March 5/2014.
Kauli hiyo ni kuamini kuwa katiba ya Zanzibar itafanyiwa marekebisho na
moja analoliamini kuwa ni kero ni sheria ya Zanzibar kuruhusu ardhi ya
Zanzibar kumilikiwa na Wazanzibari peke yao.
Waziri Samia
Suluhu Hassan, aliwaeleza wandishi hao wa habari ya kuwa anamini kuwa
katiba ya Zanzibar nayo itafanyiwa marekebisho makubwa na marekebisho
hayo yatalenga kile ambacho yeye anakiona ni kero kwa Muungano ni sheria
ya Zanzibar inayoruhusu na kulinda ardhi ya Zanzibar kutomilikiwa na
watu ambao sio Wazanzibari.
Waziri Samia Suluhu Hasan kwa
mtazamo wake yeye kuwa kero moja ya Muungano ni kutoruhusiwa kwaa
Watanzania bara kuruhusiwa kumiliki ardhi chache na ndogo iliyopo
Zanzibar.
Jambo ambalo tunaamini si kwa bahati mbaya au kama
hajuwi kuwa ardhi haikuwamo katika mambo kumi na moja ya makubaliano ya
mambo ya Muungano, kila nchi ina sheria tofauti ya umiliki na usimamizi
wa ardhi.
Bali mtazamo huu ni usaliti wa wazi wa Mapindauzi ya
mwaka 1964 ambao lengo lake kuu moja wapo ni kuigawa ardhi chache ya
Zanzibar kwa wananchi wa Zamzinar ili ilete tija na maendeleo kwao na
Taifa kwa ujumla.
Chama cha Wananchi CUF kinamini kuwa kuna
kero nyingi za Muungano kama Waziri wa Mungano kuzizungumzia kero ambazo
zimeufikisha Muungao huu pahala pabaya, na kuzua malalamiko mengi hasa
kwa upande wa Zanzibar kwa kupoteza mamlaka yake na uwezo wake kinyume
na makubaliano yaliyounda Muungano huo wa mwaka 1964 .
Leo hii
tunashuhudia tena kauli za kuendeleza dhamira ya kuipotezea Zanzibar
Utaifa wake kwa lengo la kujikweza, kujipatia umaarufu kuwafurahisha
wachache wasioitakia mema Zanzibar.
Chama Cha Wananchi CUF
kinaamini ndani ya Muungano huu wa miaka 50 kumekuwa na kasoro nyingi na
kubwa hali iliyopelekea rais wa
Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuchukua hatua ya kuunda tume ya kukusanya maoni.
Ambapo hivi sasa Bunge malum la katiba linakutana kwa ajili ya
kutengeneza katiba mpya ambayo tayari rasimu ya pili ya marekebisho
imeshatoka.
Alichokizungumza Samia Suluhu ni kuinadi ardhi ya
Zanzibar na kuiweka mnadani, na ukiondoa udhibiti huo wa ardhi kwa
Wazanzibari ambao upo kisheria ni kufungua soko kwa watu takriban
milioni 50 wenye uwezo kuivamia ardhi isiyozidi 2500 sq.km ya ardhi ya
Zanzibar kwa maslahi ya Watanzania Bara wenye ardhi zaidi ya 950.000
sq.km, hali hiyo inaonesha wazi lengo na dhamira ya kuimeza Zanzibar
HAKI SAWA KWA WOTE
Salim Abdalla Bimani
Mkurugenzi Haki/H/Uenezi/Masiliano ya Umma
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA