Lupita:Mwanamke mrembo zaidi 2014
Jarida la People limemtangaza Mkenya Lupita Nyong’o kama mwanamuke mrembo zaidi duniani mwaka 2014
Lupita ambaye alishinda tuzo ya Oscar kwa uigizaji wake katika filamu
'12 years a slave,' yuko kwenye ukurasa wa juu zaidi wa makala ya wiki
hii ya jarida hilo.
Katika orodha yake ya wanawake 50 warembo duniani,Lupita amewapiku
waigizaji maarufu akiwemo Kerry Washington, ambaye pia alishiriki katika
filamu hiyo na mwanamuziki Pink ambao walikuwa katika nafasi ya 10 na 5
mtawalia.
Stacy Kiebler ambaye alisifika sana kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
muigizaji nyota George Clooney, alishikilia nafasi ya nane.
Hatua ya Jarida la People ambalo huchapishwa kila wiki nchini Marekani
na kusomwa na karibu watu milioni 40, kumkubali Lupita kama mwanamke
mrembo duniani, ni kama tuzo kivyake kwa muigizaji huyo ambaye amegonga
vichwa vya habari nchini Marekani tangu kushinda
Mtandao wa People.com, unasema kuwa muigizaji huyo alifurahia sana
kutajwa na jarida hilo kama mwanamke mrembo hasa kwa sababu wasichana
kama yeye watapata kuwa na matumaini ya kufanikiwa maishani kama yeye.
"Nimefurahi sana na hii ni fursa kuwafanya wasichana wengine wajihisi kuwa wana uwezo wa kufiia chochote maishani mwao.
chanzo na BBC
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA