Apr 24, 2014

TAARIFA KUHUSU MOTO ULIOZUKA SHULE YA SEKONDARI IVUMWE-MBEYA:


Bweni Moja la Wavulana lenye vyumba zaidi ya Sita katika shule ya Sekondari ya Ivumwe inayomilikwa na Chama Cha Mapinduzi limeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea leo April 23 majira ya saa3 asubuhi jijini Mbeya wakati wanafunzi hao wakiwa madarsani kuendelea na masomo yao kama kawaida.

Akizungumza katika eneo la Tukio hilo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Daktari Victory Kanama amesema kuwa moto huo umeanza majira ya saa3 asubuhi wakati teyari wanafunzi wakiwa madarasani.

Taarifa za kuungua kwa moto huo zilitolewa na mmoja wa wananchi waliokuwa wakipita pembezoni mwa Mambweni hayo ambapo katika maelezo yake alieleza kuwa ameona moshi mkubwa ukitokea ndani ya mabweni hayo. 


 
wanafunzi wakikagua vitu vyao baada ya kuviokoa toka katika bweni lao

 
bweni likiwa limeteketea kabisa 
 
baadhi ya vitu vilivyonusurika 
 
tunatoa pole kwa mkuu wa shule pamoja na wanafunzi kwa matatizo haya yaliyowakuta 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA