May 13, 2014

MASKINI! KICHANGA CHATUPWA ENEO LA MTO NG'OMBE MWANANYAMALA, DAR

Kichanga kikiwa kimetupwa eneo la mto Ng'ombe Mwananyamala jijini Dar.
 
  Wakazi wa Mwananyamala wakiwa eneo la mto Ng'ombe kushuhudia tukio hilo.

MWILI wa kichanga kinachokadiriwa kuwa na siku mbili umeokotwa ukiwa umetupwa eneo la mto Ng'ombe jirani na Rasco, Mwananyamala jijini Dar.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, kichanga hicho cha kiume kimekutwa eneo hilo leo asubuhi kikiwa kwenye mfuko wa Rambo. 

Mtandao huu ulifanikiwa kuongea na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho, Bi. Husna aliyetoa rai kwa wananchi wa eneo lake kutojihusisha na vitendo viovu kama hiki, huku akiwasihi kutumia njia za uzazi wa mpango kujikinga na matatizo kama hayo.

"Nina masikitiko makubwa kwa kitendo hiki, ni bora kichanga hiki kingeletwa serikalini tukilee kuliko kutupwa eneo hili. Kama wananchi mkishindwa kuvumilia bora mtumie uzazi wa mpango," alisema Bi. Husna huku akiahidi kufanya uchunguzi wa kina kumtafuta muhusika!0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA