
Makamu Mwenyekiti wa kalbu ya Yanga SC Bw Clement Sanga (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Benki ya Posta, kulia ni mkurugenzi masoko wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa
Klabu ya Young Africans imeeingia 
makubaliano na Benki ya Posta nchini juu ya mabadiliko ya utengenezaji 
wa kadi za wanachama kutoka kwenye mfumo wa zamani (analogy) kwenda 
kwenye mfumo mpya wa kisasa (digital) ambapo sasa wanachama wake watakua
 wakitumia kadi zenye mfumo wa ATM.
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta  nchini
 Bw. Deo Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na 
viongozi na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo
 wake wa kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa 
muda mfupi.
"Badala ya wanachama kuja 
Dar es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama watakua wanaweza 
kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki ya Posta na kujaza
 fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama" alisema Deo. 
Gharama
 za kujiunga na uanchama zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya 
mwaka elfu Tshs 12,000/= ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB 
yenye logo ya timu yake ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI 
kwa huduma ya kuweka na kutoa fedha.
Naye
 Makaumu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru 
Benki ya Posta kwa kuweza kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo 
huu wa kisasa tutaweza kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi 
zaidi na taarifa zetu zitaweza  kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi
 rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye 
hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na 
mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka
 kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.
  Dar Es Salaam Time
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA