Apr 14, 2012

MTATIRO AONGOZA WAKULIMA WA KOROSHO KUDAI HAKI YAO


Hapa Ni tandahimba - mtwara, nimetoka kuongoza maandamano makubwa ya maelfu ya wakulima wa korosho yaliyofanyika jumatano 11/04/2012 . Hadi Leo msimu wa kilimo unaanza huku serikali ikiwa haijawalipa fedha za mwaka jana. Serikali haimjali mkulima hata kidogo, hata jasho lake anakopwa! Maandamano haya yaliishia kwa ofisi ya mkuu wa wilaya hon. Mwilima ambaye akiwa na ulinzi wa polisi takribani 30 wenye silaha za MOTO aliyapokea maandamano na kuwajibu wananchi upuuzi na kejeli badala ya kuwaeleza fedha zap zitalipwa lini. Baada ya kauli zake za "kishenzi", wananchi walikasirika sana na kutaka kuanza mapambano na polisi. Nikishirikiana na mhe. Katani-mwenyekiti wangu wa wilaya na mbunge aliyedhulumiwa LIVE katika jimbo hilo, tulifanikiwa kuwatuliza wananchi. Mkuu wa wilaya ambaye Ni kada namba moja wa ccm Alimshinikiza PCS atumie nguvu ATI kwa sababu wananchi wanamtukana matusi ya nguoni. OCD huyu alikuwa imara sans na alipingana na DC MWILIMA live. Baada ya DC kuwakejeli wakulima wa tandahimba juzi na Hans vijiji bingo njia zilifungwa na kumekuwa na mapambano makali sans kati ya polisi na raia. Jana, kijana wa miaka 13 alipigwa risasi iliyofunua na kumsababishia jeraha kubwa sehemu ya makalio. Vijana wengi wamekamatwa, cha kusikitisha, katika ziara niliambatana na vyombo kadhaa vya habari ikiwemo TBC Lakini hawajafanya juhudi kubwa kuwaeleza watanzania manyanyaso na mateso makubwa wanayopata wakulima wa kusini kutoka kwa serikali ya CCM. Mkulima analima bila msaada wa serikali, ananunua madawa na pembejeo kwa gharama zisizo na huruma, akishavuna mazao yake ndo serikali inajitokeza kumpangia bei kandamizi na kumpangia kampuni ambazo atapswa kuziuzia mazao kwa mkopo. Tunaelekea wapi jamani? Mkulima wa nchi Jou anaondolewa ushindani wa ununuzi kimakusudi. Wajanja wachache wanaunda kampuni zao na kuhakikisha vyombo vya dola, viongozi wa serikali na ccm wanakuwa na percentage zao kisha wanasimamia unyanyasaji huu mkubwa kwa kuwatisha wakulima na bunduki. Mkulima anakopwa halafu halipwi, tunataka nchi iingie vitami? Vita ya madaktari inatutoa makamasi, ya wakulima tutaiweza? Mbona Luna makampuni mengi tu yangeweza kulipa pesa nzuri na CASH kwa wakulima na tunayakimbia? Yaani ati serikali ndo inapigana kufa na kupona kuhakikisha makampuni yenye uwezo wa kulipa pesa nzuri kwa mkulima wa korosho hayapati nafasi hiyo. Watu binafsi wanaolipa pesa nzuri hawaruhusiwi kununua korosho. "Msababishie umasikini umtawale"!
Tunakoelekea sasa ni pabaya, ole wenu mliopewa jukumu la kuongoza, chezeeni wakati wenu, chezeeni maisha ya wavuja jasho,
Kuna siku wataamua kusema.
Julius mtatiro,
Njiani kurudi DSM.


chanzo na JULIUS MTATIRO 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA