Apr 16, 2012

TAARIFA KAMILI YA JAMES OLE MILYA KUJIENGUA CCM HII HAPA SOMA .


  ALIEKUWA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA ARUSHA JAMES OLE MILLYA AHAMMIA CHADEMA
NI MWENYEKITI

wa UVCCM, Mkoa wa Arusha,kwa miaka mitano, James Millya,
ametangaza kujiuzuru nafasi zote kuanzia Taifa hadi Mkoa na kutangaza
kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa madai
kuwa CCM imefilisika kimawazo na haitoi matumaini kwa watanzania.

Hayo ameyasema leo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye
Hoteli ya Kibo Palace, iliyopo Jijini hapa.

Alisema mara nyingi alikuwa akikemea mambo ambayo yanaweza kubomoa
chama cha CCM kwa upendo, lakini alikuwa akipuuzwa kwa sababu ya chama
hicho kuwa na kikundi cha wenyewe.


Alitaja nafasi alizoachia ngazi ni pamoja na Mjumbe kamati ya
utekelezaji UVCCM Taifa, Mjumbe kamati ya siasa Mkoa na Mjumbe
Halmashauri Kuu CCM Mkoa.

ALisema kuw ainasikitisha kuona Vijana wa UVCCM Mkoa wa Pwani, wanatoa
matamko kuwa Rais ajaye 2015 hatatoka kanda ya Kaskazini na
anayemfahamu ni Rais peke yake ambaye ni Jakaya Kikwete.

Millya alisema cha kusikitisha pale alipokemea kauli hiyo alipuuzwa na
hadi sasa Ikulu haijawahi kutoa kemeo kwa Vijana hao na wala kukataza
kauli hizo kutolewa, jambo lililompa jibu kuwa Ikulu inahusika kw
anamna moja au nyingine na kauli hiyo.

Aidha alisema kuna Vijana wengi walioko ndani ya CCM wakiishi kwa
matumaini ya kusubiri kuteuliwa nafasi ya Mkuu wa Wilaya kama sio
Mkoa, ila yeye hawezi kuishi kwamatumaini kama muathirika wa Ukimwi.

Hata hivyo alitoa wito kwa Vijana wote wenye nia ya dhati na mapenzi
mema ya nchi yao, kumfuata Chadema ambako kunatoa tumaini jipya la
maisha ya watu.

Millya ambaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM tangu 2008 hadi
sasa, aliwashukuru vijana kwa kumpa ridhaa hiyo na ataendelea
kuwashukuru, ila ameamua kwa ridhaa yake kuachia ngazi zote kwa ajili
ya ukombozi wa kweli.

Millya hivi karibuni alijitosa kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge wa
Afrika Mashari ndani ya Chama chake cha CCM, lakini alichinjiwa
baharini na kutolewa jina lake.

Wakati Kiongozi huyo akitangaza kuachia ngazi hiyo ya juu ya UVCCM,
ndani ya Chama cha CCM, Mkoa wa Arusha, Vijana mbalimbali wameonekana
kutoamini walichosikia na wengi wao wakionyesha nia ya kumfuata.
PICHA CHINI KIPINDI CHAKE YUKO CCM

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA