Jan 20, 2014

Exclusive: Nikki Mbishi aelezea kilichomo ndani ya mixtape yake 'Ufunuo', itatoka June 16 mwaka huu

 Exclusive: Nikki Mbishi aelezea kilichomo ndani ya mixtape yake

Rapper wa Tamaduni Music mwenye aka nyingi, Nikki Mbishi Zohan, Jogoo, Terabyte, Baba Malcom na nyingine ameielezea kanda mseto yake aka mixtape aliyoipa jina la ‘Ufunuo’ atakayoiachia June 16, mwaka huu.

“Kinachokuja ni Ufunuo, ni mixtape sio ya gospel, sio ya kidini na wala haielezei ukristo wala uislam wala nini.” Nikki Mbishi ameiambia tovuti ya Times Fm.

“Ila kilichopo humo, Ufunuo ni kuwahabarisha watu mambo mpya yanayokuja kutokea. Ama ni utabiri wa majirio, yaani kwamba vitu vitakavyokuja…yaani kama maono yaani.”Ameeleza.

Amesema amepanga kutoa mixtape hiyo June 16 ambayo itakuwa siku ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika, na kwamba siku hiyohiyo itakuwa ni siku ya kuzaliwa mwanae ‘Malcom’.

'Play Boy' hit maker amesema ameamua kuachia mixtape hiyo ikiwa ni miezi kadhaa tangu aachie mixtape nyingine kwa kuwa anaona ni bora afanye mengi wakati bado ana nguvu.

“Mi nafikiri nipo kwenye nguvu ya kuweza kuvifanya hivi vitu kwa wingi kadri ninavyoweza. Kwa hiyo kama muda ndio huu basi niacheni nifanye. Kwa sababu muda ukifika na ubongo ukichoka na wasanii ujue ni wengi huwezi kufanya hivyo vitu.

“Kwa hiyo cha msingi kama unapata mashairi unaandika na unarekodi, unapata studio time na nini…basi acha ufanye.” Amefunguka Zohan.

chanzo na times fm

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA