Jul 4, 2012

TBL YAKABIDHI 'MPUNGA' WA UCHAGUZI YANGA

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steven Kilindo (kulia) akimkabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni 20, Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa (kushoto) katika hafla fupi ya kukabidhi hundi hiyo iliyofanyika makao makuu ya TBL, Ilala Dar es Salaam asubuhi ya leo.
TBL imetoa fedha hizo kwa ajili ya uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo, uliopangwa kufanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Julai 15, mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya mkataba wa udhamini baina ya Yanga na Kilimanjro Premium Lager Beer, inayozalishwa na TB L.  
Wengine nyuma yao, kutoka kulia ni Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili, Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah, Meneja wa Bia ya Safari Lager aliyemuwakilisha George Kavishe, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro aliye safarini na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Jaji John Mkwawa.  

Angetile akielezea jambo, kulia kwake ni Kaswahili

Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu katikati akiwa na 'vimwana' Dina Ismail kulia na Elizabeth Mayemba kushoto

Mwesigwa akiondoka TBL na begi lake dogo likiwa na 'mahela', kulia ni Clara Alphonce wa Mwananchi

Mkurugenzi wa Executive Solutions, Aggrey Marealle aliyekuwa mwongoza shughuli hiyo


Oscar Shelukindo katikati akimuwakilisha George Kavishe. Kulia ni Kilindo na kushoto Mwesigwa

Jaji Mkwawa akitafakri jambo

Mwesigwa akizungumza   picha na habari kwa niaba ya   BIN ZUBEIRY  kwa habari zaidi tembelea www.http://bongostaz.blogspot.com                                 
0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA