Asalaam Alaykum!
Saa 4 asubuhi nilifika Central Police kusimamia mahojiano yake na
Polisi kwa mujibu wa haki za mtuhumiwa nilionana na msaidizi wa ZCO
daada ya utambulisho na kumfahamisha haki zake wakati wa mahojiano
alihojiwa. Ukiacha namna alivyokamatwa mpaka naondoka polisi saa 10
kasoro alikuwa ktk hali nzuri na polisi akiwa kituoni hawakumfanyia
lolote lililokinyume na haki za mtu aliyechini ya ulinzi.
Sheikh anatuhumiwa na mambo yafuatayo:-
1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
i. kwanini waliandamana
ii. nani aliandaa mabango
iii. kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda kumng'oa Mufti na Ndalichako
iv. nani aliandaa maandamano
Sheikh alikiri kuhamasisha maandamano na pia alikubali ujumbe
uliuokuwa katika mabango ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa
yeye hajui nani aliyaandika hayo mabango. Kuhusu Mufti na Ndalichako
alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya
waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za
Kiislamu na yeye ni katibu wake.
2. Kuvamia kiwanja cha chang'ombe
Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale
kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa
eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi aende kushitaki mahakama ya ardhi na
waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa
amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.
3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu
4. Vurugu mbagala.
Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu
malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa
umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi
kasoro hivi toka saa nne asubuhi.
DHAMANA.
Baada ya
mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano
zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo
liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw.
Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda
Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi
kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema
wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP.
Lakini zaidi akasema kwa
kuwa issue ya mbagala kuna watu wameshitakiwa kwa armed robbery kosa
ambalo halina dhamana si vizuri kumpa dhamana sasa kwani huenda katika
upelelezi wao wanaweza kumuunganisha na washitakiwa wa armed robbery
mbagala. Kwa ufupi hiyo ndio hali iliyokuwepo.
NAOMBA WAISLAMU WAAMBIWE
WAWE NA SUBIRA WAKATI HUU WASIFANYE LOLOTE LITAKALOWAPA NAFASI MAADUI WA
UISLAMU MANENO YA KUSEMA
Maasalamu!
By Brother Juma Nassoro - Wakili
1. Kuhamasisha maandamano kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani. Wakati wa mahojiano walitaka kujua yafuatayo:-
i. kwanini waliandamana
ii. nani aliandaa mabango
iii. kwanini walisema kuwa baada ya maandamano yale wataenda kumng'oa Mufti na Ndalichako
iv. nani aliandaa maandamano
Sheikh alikiri kuhamasisha maandamano na pia alikubali ujumbe uliuokuwa katika mabango ulikuwa umebeba hisia za waislamu. Isipokuwa yeye hajui nani aliyaandika hayo mabango. Kuhusu Mufti na Ndalichako alisema wanastahili kuondolewa kwasababu ya kuongoza kwa dhulma dhidi ya waislamu. Pia alisema maandamano yaliandaliwa na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na yeye ni katibu wake.
2. Kuvamia kiwanja cha chang'ombe
Hapa alijibu kuwa huo ni mgogoro wa ardhi na waislamu wapo pale kwasababu ni kiwanja cha waislamu. Na kama kuna mtu anadai amevamiwa eneo lake huo ni mgogoro wa ardhi aende kushitaki mahakama ya ardhi na waislamu wapo tayari kufika mahakamani kujibu. Pia alikiri kuwa amehusika ktk ujenzi wa msikiti unaojengwa ktk eneo hilo.
3. Kuhamasisha maandamano kidongo chekundu
4. Vurugu mbagala.
Haya mawili ya mwisho hakuhojiwa kwasababu mafaili yanayohusu malalamiko hayo yalikuwa hayajafika central lakini vilevile muda ulikuwa umeenda sana. Kwani mpaka tunamaliza mahojiano ilikuwa ni saa kumi kasoro hivi toka saa nne asubuhi.
DHAMANA.
Baada ya mahojiano niliomba apatiwe dhamana na kesho afike polisi kwa mahojiano zaidi. Polisi waliokuwa wanamhoji walikataa kwa hoja kuwa suala hilo liko kwa viongozi wakuu wa jeshi la polisi. Waliomba nikamwone ZCO Bw. Msangi, yeye alisema hawezi kulitolea maamuzi akanitaka nimwone Kamanda Kova. Nilienda kuonana na Kamanda Kova naye aliniambia kuwa hawawezi kutoa dhamana mpaka amalize mahojiano yaliyobaki. Na vile vile alisema wanasubiri wapate ushauri toka ofisi ya DPP.
Maasalamu!
By Brother Juma Nassoro - Wakili
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA