AZAM YAIPELEKA YANGA BAGAMOYO
Kikosi cha wachezaji 26 wa timu ya Young Africans kinaingia kambini
leo mchana katika Hoteli ya KIROMO iiliyopo pembeni kidogo mwa mji wa
Bagamoyo tayari kwa maandalizi ya mchezo wa ligi Kuu ya Vodacom siku ya
jumamosi dhidi ya timu ya Azam FC katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam.
Baada ya kuichapa timu ya African Lyon kwa mabao 4-0 katika mchezo
uliochezwa mwishoni mwa wiki, Young Africans itashuka dimbani
kuhakikisha inaondoka na ponti zote 3 ambazo zitaifanya iendelee
kuongoza msimamo wa ligi kuu ya Vodacom (VPL) na hatimaye kutwaa Ubingwa
huo.
Kocha Mkuu wa Yanga mholanzi Ernest Brandts amesema kuwa
kikosi chake kipo fit kuelekea mchezo huo wa jumamosi, na anaamini
mchezo huo ndio utatoa taswira halisi za msimamo wa ligi kuu ya VPL
kuelekea kutwaa Ubingwa.
Namshukuru mwenyezi mungu, kikosi changu
kipo katika hali nzuri, wachezaji wote 26 nimekua nao pamoja wakifanya
mazoezi kwa nguvu, wachezaji wote wanaonyesha viwango vya hali ya juu,
hali inayonipa fursa ya kupata nafasi ya kumtumia mchezaji yoyote katika
mchezo huo 'alisema Brandts'
Young Africans inaongoza msimamo wa
VPL kwa kuwa na pointi 36 huku ikiwa imecheza michezo 16, imeshinda
jumla ya michezo 11, imetoka sare michezo mitatu (3) na kupoteza michezo
miwili (2) huku ikiwa imefunga jumla ya mabao 33 na kufungwa mabao 12
tu.
Nafasi ya pili inashikiliwa na timu ya Azam FC yenye pointi 33
ikiwa na mabao 27 ya kufunga na ikiwa imefungwa mabao 14 na kesho
itashuka dimba la Chamanzi kucheza na timu ya JKT Ruvu katika muendelezo
w amichezo ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Katika mchezo huo wa jumamosi
Young Africans inahitaji ushindi ili kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi
Kuu ya Vodacom pia itakua ni kuendeleza ushindi dhidi ya timu hiyo ya
waoka mikate wa Bakhresa kwani michezo miwili ya mwisho watoto wa
Jangwani waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Habari njema kuelekea
katika mchezo huo ni kuwa kikosi hakina mchezaji majeruhi hata mmoja
hali inayopelekea kuwa na maandalizi mazuri ya mchezo huo wa jumamosi
dhidi ya timu ya Azam FC.
Chanzo na http://www.youngafricans.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA