Mar 21, 2013

RIDHIWANI KIKWETE ATEULIWA MWENYEKITI WA UJENZI WA MAFIA

 

Ridhiwani Kikwete akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa eneo la Mafia


Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Sports Club alhaj Yusuf Manji leo amemtambulisha wakili Ridhiwani Kikwete kuwa mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa kitega uchumi katika eneo la klabu lililopo makutano ya Mafia/Nyamwezi  eneo la Ilala jijini Dar es salaam.

Akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu Manji amesema uteuzi wa Ridhiwani umezingatia uwezo wake kwa taaluma yake, na moyo alionao katika kujitolea katika kazi mbali mbali za klabu ya Yanga.

"Wote tunamfahamu Ridhiwani amekua ni mwanachama wa Yanga kwa muda mrefu, amekua akijitoa katika kazi mbali mbali za maendeleo ya klabu, hivyo tumeona ni vizuri kumpa fursa hiyo ili aweze kusaidia katika kuleta maendeleo ya klabu" alisema Manji

Katika kamati hiyo ambayo Ridhiwani ameteuliwa , amepewa fursa ya kuteua/kuchagua wajumbe atakaoshirikiana nao katika ujenzi wa kitega uchumi hicho katika mtaa wa mafia, pia atakua na uwezo wa kuongeza wajumbe au kupunguza kulingana na mahitaji kwa kipindi hicho.

Mara baada ya kutambulishwa kwa wanachama na waandishi wa habari, Ridhiwani alisema anashukuru kwa mwenyekiti wa klabu ya Yanga Manji kumteua kushika nafasi hiyo na kuahidi kuwa atajitahidi kadri ya uwezo wake kuhakikisha ujenzi huo unafanikiwa.

 "Nitakaa na kuangalia ni wajumbe gani ambao tutaweza kukaa pamoja na wajenzi (wakandarasi) ili kuweza kufanikiwa katika ujenzi wa kitega uchumi, kwani napenda eneo hilo liwe sehemu ambayo litasaidia katika uchumi wa klabu" alisema Rdihiwani 

Aidha Ridhiwan aliendelea kusema kuwa Kiwanja cha mafia kimekuwepo kwa mda mrrefu bila ya kufanyiwa muendelezeo, ila naamini tutajitahidi ili kuweza kuhakisha historia inajengwa kwa kubadili eneo hilo na kuwa sehemu ya kivutio na ya kuiingiza pesa klabu.

Ridhiwani mwisho alimalizia kwa kusema hawataishia katika ujenzi wa kiwanja cha mafia tu bali wataweka mipango kuhakikisha kuwa hata katika matawi ya Yanga sehemu mbali mbali wanaweza kuwekeza na kujenga majengo ambayo yatasaidia katika kuendeleza uchumui wa klabu.

chanzo na http://www.youngafricans.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA