Feb 14, 2013

YANGA YAZIDI KUCHANJA MBUNGA, YAICHAPA AFRICAN LYON 4-0

 
Mabingwa wa kombe la Kagame timu Young Africans leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa timu ya  African Lyon jumla ya mabao 4-0, katika mchezo uliofanyika jioni hii katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
 
Young Africans ambayo inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 36 na mabao 33 ya kufunga, iliingia uwanjani kwa ajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo imefanikiwa kuzipata.
 
Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi, na katika dakika 15 za kwanza washambuliaji wake Hamis Kiiza, Saimon Msuva na Jerson Tegete walikosa nafasi za kufunga mabao ya wazi ya mapema, kufuatia kutokua makini katika umaliziaji.
 
Jerson Tegete aliwaiunua mashabiki wa Yanga katika dakika ya 21 baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza kwa kichwa akimalizia pasi safi iliyopigwa na mlinzi wa pemebeni David Luhende ambaye alipanda kuongeza nguvu mashambulizi.
 
Yanga iliendela kuutawala mchezo na hasa sehemu ya kiungo, ambapo Haruna Niyonzima, Athumani Idd Chuji, Frank Domayo waliweza kuitawala sehemu hiyo ya katikati hali iliyopelekea wachezaji wa African Lyon kuutafuta mpira kwa tochi.
 
Dakika ya 42, Jerson Tegete tena aliipatia Young Africans bao la pili kwa staili ya peke, baada ya kuupiga kwa kisigino mpira wa krosi uliokuwa umepigwa na Haruna Niyonzima na kumfanya mlinda mlango wa African Lyon Abdul Seif na walinzi wake wasijue cha kufanya.
 
Saimon Msuva alitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini mipira hiyo ilipowakuta wafungaji hawakua katika nafasi nzuri ya umaliziaji hali iliyoplekea kukosa mabao mengine ya wazi katika kipindi cha kwanza. 
 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 2-0 African Lyon.
 
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuutawala mchezo hali iliyopelekea kujipatia penati dakika ya 48 ya mchezo, kufuatia walinzi wa African Lyon kuzidiwa na kiungo Haruna Niyonzima hali iliyowapelekea kumcheza madhambi mchezaji huyo ndani ya eneo la hatari, mwamuzi aliamuru ipigwe penati ambayo iilipigwa na Hamis Kiiza ambaye alikosa penati hiyo.
 
Kocha wa Yanga Ernest Brandts alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Didier Kavumbagu, Said Bahanuzi, na Nizar Khalfani ambao walichukua nafasi ya Hamis Kiiza, Jerson Tegete na Saimon Msuva.
 
Mbadiliko hayo yalizidi kuongeza kasi ya mashabuluzi langoni mwa African Lyon kwani dakika ya 70, Didier Kavumbagu aliipatia Yanga bao la tatu kwa mkwaju wa penati kufuatia mlinzi wa African Lyon Obina Salamusasa kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
 
Dakika ya 80 Nizar Khalfani aliipatia bao la  nne ka ustadi mzuri wa umaliziaji, akimalizia pasi ya Said Bahanuzi ambaye aliwazidi ujanja walinzi wa African Lyon na kupiga krosi hiyo iliyowapita walinzi na mlinda mlango Juma Abdul.
 
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 4 - 0 African Lyon

Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake  kupata kwa ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza washambuliaji wangu hawakuwa makini lakini kipindi cha pili timu ilibadilika sana hali iliyopelekea kuutawala mchezo kwa kipindi chote na kuongeza mabao mawili ya haraka.
 
Baada ya mchezo huu wa leo kikosi cha Young Africans kitaendelea na mazoezi yake kesho asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya timu ya Azam FC februari 23 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva/Nizar
 Khalfani, 8.Frank Domayo, 9.Jerson Tegete/Didier Kavumbagu 10.Hamis Kiiza/Sadi Bahanuzi, 11.Haruna Niyonzima
 
African Lyon: 1.Abdul Seif, 2.Yusuf Mlipili, 3.Sunday Bakari, 4.Ibrahim Job, 5.Obina Salamusasa, 6.Abdulehan Gulam, 7.Amani Kyata, 8.Mohamed Samata, 9.Idd Mbaga, 10.Bright Ike, 11.Adam Kingwande
chanzo  http://www.youngafricans.co.tz/
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA