LIWALE: WATOTO WADOGO WABAMBIKIZIWA KESI YA "UNYANG'ANYI" WA KUTUMIA SILAHA.
Mtatiro akiteta jambo na watoto hao
Hapa wakijieleza mbele ya Mtatiro wakiwa mahakamani
Watoto SAID HASSAN BADI, 14 (Kushoto kwangu) na SALAMA HASHIM MBWANA,
14 (Kulia kwangu) - (wote wanafunzi wa kidato cha kwanza) wakiwa
mahakama ya wilaya ya LIWALE mara baada
ya kusomewa mashtaka kwenye kesi zaidi ya tatu. Katika kesi moja watoto
hawa wanatuhumiwa kuvamia duka, kulivunja, kuona na kumtishia mwenye
duka (mwanaume) watamuua kwa silaha.
Nilipoongea na watoto
hawa nilishangaa sana, huyo wa kiume anasema siku ya matukio ya wananchi
kufanya vurugu yeye alikuwa anaangalia mpira, aliposikia milio ya
risasi majira ya jioni alikimbia kutoka ukumbini, njiani akakutana na
mjomba wake ambaye ni diwani wa CCM, mjomba wake akamuuliza anakimbia
nini? Akamjibu kuwa ameambiwa kuwa kuna vurugu hivyo anakimbilia
nyumbani. Diwani wa CCM akamwambia anawajua vijana waliomjulisha kuhusu
vurugu? Kijana huyu akajibu hawajui, ndipo mjomba mtu(diwani) akaanza
kumpiga makofi, na mwisho wa siku kijana huyu akakimbilia kwao.
Keshoye akaamkia shuleni, akiwa shuleni mjomba wake akaja na polisi,
wakamkamata. Hajui lolote kuhusu matukio hayo lakini anasomewa shtaka la
kuona kwa kutumia silaha usiku wa manane.
Huyu
SALMA(msichana), anasema siku moja baada ya matukio ya LIWALE, polisi
walifika nyumbani kwao(Yeye Salma na mama yake wanasimamia nyumba ya
ndugu yao yenye wapangaji). Polisi walipofika wakamkamata mpangaji mmoja
na kusachi chumba cha mpangaji huyo. Baadaye polisi wakaondoka na
mpangaji huyo pamoja na DRYER ya Saloon na kiti cha
Saloon(vinavyosemekana kuwa vya wizi).
Baada ya muda kidogo,
polisi wakarudi na wakaanza kumpiga sana msichana huyu na mama yake,
wakawakamata na kuwaweka Rumande. Yule mpangaji alokutwa na vitu vya
wizi aliachiwa kesho yake na hajapandishwa kizimbani.
Hadi mtoto huyu na mama yake wanafikishwa mahakamani hawakuwahi kujua kosa lao ni nini.
Wamefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kesi 4 tofauti. Katika kesi
mojawapo, mtoto huyu anatuhumiwa kwa kesi ya unyang'anyi wa kutumia
silaha na haina dhamana.
Chama kimechukua hatua za dharura za
kuweka mawakili ili wananchi wanaobambikiziwa kesi wanusurike.
Inasikitisha sana. Polisi watumika vibaya.
habari kutoka kwenye account ya facebook ya Mtatiro
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA