May 4, 2013

MECHI YA AZAM KUONEKANA CLOUDS TV

Kwa bahati mbaya kutokana na matatizo ya kiufundi Star TV walioko mkoani Mwanza hawataweza kurusha mchezo kati ya Azam FC na AS FAR, kwa hiyo Kandarasi hii wamepewa Clouds TV, lakini Kiss FM na Radio Free Afrika masafa ya kati watawaletea matangazo haya ambapo mtangazaji wao Hemed Mvula tayari ameshatua mjini Rabat. Mechi itaanza saa moja kamili usiku kwa majira ya Tanzania. Usikose