NGASA ATAMBULISHWA RASMI YANGA
Katibu Mkuu wa klabu ya Young Africans Lawrence Lawrence Mwalusako
leo amemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari mchezaji Mrisho Ngasa
ambaye amerejea katika klabu yake ya zamani kufuatia kumalizika kwa
mkataba wake wa miaka miatatu (3) dhidi ya timu ya Azam FC.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu Mwalusako
amesema Ngasa amerejea katika timu yake, alikuwa mchezaji wetu kwa muda
mrefu kabla ya kuhamia katika timu ya Azam FC ambako alitumikia mkataba
wa miaka 3 uliomalizika mwisho mwa msimu huu.
Naye mwenyekiti wa
mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema anashukuru kwa
Ngasa kuamua kurudi nyumbani, kwani amekuwa mchezaji anayejitolea kwa
moyo wake wote katika timu zake zote alizokuwa akichezea hali
iliyompelekea kuendelea kuwa katika kiwango cha hali ya juu.
Kwa
kweli mimi binafsi nimefurahi kijana kurejea nyumbani, amerejea katika
timu inayomjali, inamsikiliza alisema Bin Kleb huku akimalizia kwa
kusema kuwa Ngasa ataitumikia Yanga kwa mkataba wa miaka 2.
Aidha
Ngasa mwenyewe amewashakuru wapenzi, washabiki na wanachama wa klabu ya
Yanga kuwa naye kwa nyakati zote, nilipohamia Azam walikua
wakishangilia, nilipohamia Simba pia walikuwa wakinipa moyo na
kunishangilia pia.
Nimeamua kurudi katika timu yanga ya zamani
sababu ndio sehemu pekee wanaponisikiliza na kunithamini, timu
niliyotoka pamoja na kucheza kwa moyo wangu wote bado viongozi wake
hawakua na imani na mimi hicho ndo kilichonipelekea kurudi katika timu
yangu ya Yanga.
Ngasa anakua mchezaji wa kwanza kusajiliwa na klabu
ya Yanga kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi kitachoitumikia
Yanga katika msimu ujao.
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO (DMNM)
EVER FORWARD BACKWARD NEVER (EFBN)