Jul 19, 2013

HIKI NDICHO ALICHOSEMA JANUARY MAKAMBA BAADA YA MNYIKA KUWEKA NAMBA YAKE YA SIMU

John Mnyika kaweka namba yangu ya simu ya mkononi ili watu wanipigie na kutukana. Nadhani ni siasa isiyo ya kistaarabu. Hadi sasa nimepata messages zaidi ya 600. Sio sahihi kabisa.

Wabunge WOTE tulishindwa kupitisha maamuzi yenye maslahi kwa mtu wa kipato cha chini. Harakati za mitandaoni haziondoi ukweli huo. Vilevile, kodi hii imepitishwa tarehe 29 Juni 2013. Kwa Mbunge ambaye alikuwa na wajibu wa kulipinga siku hiyo na kulisemea kuanzia tarehe 30 Juni 2013 kuamka leo na kutapatapa mitandaoni ni unafiki mkubwa na ni siasa za kuangalia upepo unapovuma na ni unafiki mkubwa. Namheshimu Zitto Kabwe kwasababu alitoa kauli immediately ya kusema anaona aibu kuwa sehemu ya Bunge hili na kwamba wawakilishi wa wananchi wamewaangusha wananchi. Mwenzake John Mnyika anajitoa fahamu na kufanya harakati kupitia press releases.


Suluhisho hapa sio kulumbana wala kutupiana lawama. Suluhisho ni kurudi Bungeni na kubadilisha pale tulipokosea. Sio kutafuta umaarufu mitandaoni. Kunapotokea kosa, tunasahihisha haraka then we move on. Siasa sio kwenye kila jambo.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA