Serikali nchini Kenya imetangaza kufungwa kwa shule zote za msingi za
umma huku walimu wa shule za umma za msingi na sekondari wakisitisha
mgomo wao.
Waziri wa elimu prof Profesa Jacob Kaimenyi amesema
kuwa shule hizo zitabakia kufungwa kwa muda usiojulikana. Ameshutumu
walimu akisema kuwa mgomo wao ulikuwa kinyume cha sheria.
Zaidi ya
walimu laki mbili na arobaini wamesusia kutoa mafunzo kwa wanafunzi
wakidai nyongeza ya asili mia mia tano ya mishahara waliyoahidiwa na
serikali mwaka wa 2007.
Pia wanataka kuongezewa marupurupu ya
usafiri, ya nyumba na matibabu. Serikali imesema kuwa wazazi wataarifiwa
juu ya siku ya kufunguliwa tena shule.
Waziri huyo wa elimu
amesema kuwa wizara yake itafanya mipango maalum kwa ajili ya wanafunzi
wa darasa la nane wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa kitaifa chini ya
miezi minne ijayo.
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP
2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi
ya New B...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA