CUF WAIMBO SERIKALI ILIFUNGIE GAZETI LA TANZANIA DAIMA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 18/07/2013
Mhariri
CUF TUNASHANGAZWA NA JINSI SERIKALI INAVYOSHINDWA KULICHUKULIA HATUA
GAZETI LA TANZANIA DAIMA KWA KUENDELEZA UCHOCHEZI WA KIDINI.
CUF-Chama cha Wananchi kinasikitishwa sana na kitendo cha uchochezi wa
Kidini unaofanywa na Gazeti la Tanzania Daima chini ya Muandishi George
Maziku, kufuatia habari iliondikwa leo Tarehe 18/07/2013 toleo na 3149 .
Aina hii ya uchochezi na Chuki ya Kidini anayoiendeleza bw, Maziku
chini ya usimamizi wa Mmiliki wa Gazeti la Tanzania Daima na Mhariri
wake, kwa maslahi ya Kisiasa tu, yatatupeleka mahala pabaya sana kama
Taifa.
CUF-Chama cha Chama Wananchi tunashangazwa na tuna hoji juu
ya lengo na Dhamira ya Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake nini
juu ya muendelezo wa habari wanayoitoa kwa muda wa miezi miwili sasa ?
Habari hii ina lenga nini ? Kwamba Viongozi wa Kisiasa wanaotokana na
Dini ya Kiislam hapaswi kujumuika na Waislam wenzao kwenye Nyumba za
Ibada ? Au waislam hawapaswi kujadili Maendeleo ya Taifa lao ?
CUF-Chama cha Wananchi tunaona Lengo la Gazeti la Tanzania Daima na
Muandishi wake ni kupandisha hasira za Waislam kwa mtazamo wa Ubaguzi wa
Kidini kupitia tasnia ya Habari na hivyo kuleta machafuko yasiokuwa ya
lazima. Hata hivyo ikiwa lengo ni kuondosha Dalili za Udini kwenye mambo
ya Siasa, hivi Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake hawakuona
Waraka wa Uchaguzi wa Mwaka 2010 uliotolewa na Kanisa Katoliki na kupewa
jina la IIani ya Uchaguzi wa Kanisa Katoliki ? Waraka ambao uliwataka
Wakristo kuichagua Chadema na wagombea wake, Sio hivyo tu Waraka huo
ulikwenda mbali zaidi na kuwatahadharisha Wakristo wasichague CUF na CCM
na kuvifananisha Vyama vya CUF na CCM ni sawa na Chui waliovaa Ngozi ya
Kondoo kwa Kanisa.
Waraka huo ulipingwa vikali sana na Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru. Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake walikuwa wapi
? Mbona hatukuona waandike KANISA LA CHOCHEA UDINI ? Kama hiyo
haitoshi, hivi Gazeti la Tanzania Daima na Muandishi wake mbona
hawakumkemea wala kuandika kuhusu Askofu Kakobe alipokua anampigia debe
Mgombea wa Urais kupitia Chadema 2010 tendo ambalo lilikuwa linaonyeshwa
wazi wazi kupitia Star Tv.
Kama hiyo haitoshi katika uchaguzi mdogo
wa madiwani uliofanyika jijini Arusha na Chadema kushinda wafuasi na
viongozi wake kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS) kuwa YESU AMESHINDA
hilo nalo hukuliona?
Kama hiyo pia haitoshi ? Mwaka huu Mery Nagu
amekwenda kusali Kanisani na kuwataka Wakristo wajitokeze kwa wingi
kutoa maoni yao kuhusu katiba mpya na kuwataka waumini hao wapinge mambo
yote yanayotakiwa na kikundi kidogo cha baadhi ya watu kwa maslahi ya
Kanisa, je huu haukuwa UDINI ? Lowasa kila kukicha yupo Makanisani na
Misikiti na anatoa Fedha anatoa je hilo sio tatizo ?
Kwa
mkusanyiko wa hoja zote hizi , CUF –Chama cha Wanainchi kinashindwa
kuelewa kwanini Serikali haioni hatari inayofanywa na Gazeti la
Tanzania Daima na Muandishi kwa tendo hili la Uchochezi wa Kidini ?
Ikiwa Serikali iliweza kuzifungia Radio Imani na Radio Maria zote
zikiwa zinarusha matangazo yake kwa Malengo ya Kuendeleza Dini zao,
inashindwaje kulitazama Gazeti hili la Tanzania Daima ? Hivi Serikali
inasubiri nini ? mpaka hao Waislam wanaotumiwa kuwa wadini waje juu na
kuleta vurugu ? Ni busara kwa Serikali kulitazama jambo hili kabla
halijalet madhara.
CUF-Chama cha Wananchi kinaishauri Serikali
kulitazama kwa makini jambo hili, kabla halijaleta madhara, uandishi wa
aina hii ndio uliosababisha Mauaji ya Kimbali. Uandishi wa Uchochezi
unaolenga kuligawa Taifa kwa misingi ya Ukabila au Udini ni uandishi
hatari sana kwa Taifa letu. Bahati mbaya Tanzania Daima hawajui au
wamesahau kwamba kwa chuki ya Kidini wanayojitahitahidi kuipandikiza
ndani ya Taifa letu kwa nguvu ya Tasnia ya Habari, haitawaacha SALAMA
wao kama Gazeti wala Muandishi wa Habari hiyo ya Uchochezi na wanapaswa
kutambua kwamba kwa kufanya hivyo tu, basi wanainunua hatari ya Taifa
letu kwa gharama kubwa.
Malengo ya Kisiasa yasije kulisambaratisha Taifa
letu eti kwa sababu tu Chadema ichukue Nchi. Mnaweza kufikia Lengo la
kuchukua Nchi kwa Mtazamo na Mkakati huo wa Kidini, kama ambavyo
mnaendlea kufanya, lakini mjue kwamba mtachukua Nchi isokuwa salama.
Maana mtakuwa mmeigawa Nchi kwa Matabaka ya Udini.
Kama kweli wewe
ni mwandishi mahiri na mpenda amani katika nchi, tafadhali soma kitabu
cha KANISA KATOLIKI NA SIASA YA TANZANIA BARA KUANZIA MWAKA 1953 HADI
1985 kilichoandikwa na Dr. John C. Sivalon na uje na uchambuzi wa dini
uliomo katika kitabu hicho.
CUF- Chama cha Wananchi kinalitaka
Gazeti la Tanzania Daima , kuanzia Mmiliki wake, Mhariri wake na
Muandishi wa Habari hizi, ambae mara huandika kwa mtindo wa Makala ,
mara huzipa uzito mkubwa kadri anavyoona inafaa kwa utashi wa Kisiasa au
Udini wake, kujitazama upya juu ya hili wanalolitengeneza kama
litaiweka Nchi yetu katika eneo salama.
Mwisho CUF-Chama cha Wananchi kinaitaka Serikali kuchukua hatua juu ya Uchochozi huu.
Imetolewa na
Abdul Kambaya , Naibu Mkurugenzi wa Habari, Haki za Bainaadam na Mahusiano ya Umma
0719 566 567
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA