Hii ndio idadi ya filamu alizoigiza mzee Majuto, na kipato anaochopata kwa mwezi.
Umeshawahi kujiuliza Mzee Majuto anaweza kuwa anaingiza shilingi
ngapi kwa kuigiza kwenye movie zake za vichekesho ambazo mpaka sasa
ndio zinashika namba 1 kwa mauzo Tanzania?
Akizungumza na mtandao wa millardayo Mzee majuto amesema ‘kwenye
movie za kuigiza sasa hivi kama mtu akitaka kunishirikisha ni lazima
unilipe milioni nane kutoka milioni 2 au tatu nilizokua nazikusanya
mwanzoni, hii bei nimeibadili kuanzia mwezi September 2013, mimi kadri
ninavyocheza movie nyingie za kushirikishwa ndio nazidi kujipunguzia
kipato changu kwa mwezi kutoka kampuni ya STEPS iliyoniajiri’
‘Mpaka sasa nimecheza movie zaidi ya 600 toka nimeanza kuigiza
za kushirikishwa na zangu mwenyewe, nilianza kulipwa zaidi ya milioni
moja kwenye movie toka mwaka 2007/2008 baada ya kuwa na kampuni ya Ally
Riyami ambae alikua ananilipa shilingi laki sita kwa kila movie ya
Comedy kwa hiyo kwa mwezi napata mpaka kwenye milioni 6 au saba kutokana
na idadi ya movie nitakazoigiza’ – Mzee Majuto
‘kwa sasa hapa Steps nalipwa kuanzia milioni 17 mpaka 20 kwa
mwezi, ni malipo mazuri sana ambayo napata kila mwezi na nimepangiwa
kucheza movie 9 kwa mwaka lakini kule Ally Riyami kwa mwezi ndio nilikua
nacheza hizo movie 10, yani unacheza movie nyingi mpaka unasikia
kizunguzungu…. kwa sababu nilitakiwa kucheza movie 1 kila baada ya siku
tatu ila kwa sasa kwenye mkataba wa Steps nacheza movie moja ya kampuni
na moja ya nje ya kampuni, maisha mazuri’ – Mzee Majuto
chanzo na http://www.bongomovies.com
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA