Oct 8, 2013

Mabasi yaendayo Mikoani yamegoma asubuhi ya leo

Mabasi yaendayo mikoani leo asubuhi yamegoma kufanya safari zake kama ilivyo ratiba zake za kawaida, kwa madai kwamba walikuwa kwenye mgomo. Mwandishi wetu John Chacha alipofika katika Kituo kikuu cha mabasi Ubungo alikuta mabasi yote yakiwa yamepakia abiria lakini hayakuwa yametoka kufuatia wamiliki wa mabasi hayo kuwakataza madereva kuyatoa mabasi hayo kama ilivyo kawaida. 
Mabasi hayo yamegoma kufuatia mgomo wa malori uliosababishwa na ongezeko la tozo la asilimia 5 katika mizani. 
 
Taarifa kamili ya John Chacha hii hapa:
 
 
Baadhi ya abiria wakiwa njia panda katika kituo cha mabasi Ubungo

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA