Video: Kontena lenye vitu vya ajabu na vya kichawi lapatikana Kenya
Kontena lililokuwa na mzigo wa vitu vya ajabu limepatikana kwenye bandari ya Mombasa jana. Mzigo
huo ulikuwa umefungwa kwenye katoni 10 kubwa zilizokuwa na mafuvu ya
plastic ya binadamu, miguu, mikono, maiti (za plastic) na vitu vingine
vya ajabu ajabu.
Afisa wa mamlaka ya mapato ya Kenya
alisema vitu hivyo viliagizwa kutoka China na mwanasiasa maarufu wa
Kenya. Alisema mzigo huo haujaruhusiwa kutoka bado. Inasemekana vitu hivyo vinahusiana na mambo ya kishirikina.
Uchunguzi kuhusu mzigo huo umeanza kufanyika na yule aliyeuingiza nchini humo atatajwa. Miongoni mwa vitu hivyo ni pamoja na ile inayomuonesha mtu akihangaika na kulia kwa maumivu makali na anashambuliwa na panya.
chanzo na times fc
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA