Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya
Vodacom Young Africas leo jioni wamefanya mazoezi katika viwanja vya
shule ya seminari ya wakatoriki Ntungamo - Kashura pembeni kidogo ya mji
wa Bukoba kujiandaa na mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya wenyeji
Kagera Sugar katika uwanj wa Kaitaba.
Kelvin Yondani aliyeripotiwa na
chombo kimoja cha habari kwamba ameondolewa kwenye timu taarifa hizo
hazina ukweli kwani mlinzi huyo kisiki wa kati ni miongoni mwa wachezaji
waliofanya mazoezi jioni ya leo pamoja na kikosi cha Yanga.
Young
Africans ambayo iliwasili katika mji wa Bukoba majira ya saa 5 asubhi
ikitokea jijini Dar es salaam ambapo ilipitia jijini Mwanza kabla ya
kutua kwenye mji huu ambao una mandhari mazuri na hali ya hewa safi.
Kocha
mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts ametumia muda wa masaa mawili
kuwafua vijana wake 21 ili kuwa fit kuelekea mchezo huo wa jumamosi
ambao ni muhimu kwa Yanga kupata pointi 3 ili kujiweka katika mazingira
mazuri.
Timu ilipolekelea uwanja
wa ndege na umati mkubwa wa wapenzi na washabiki wa Yanga ambao walisema
wamefurahia kuiona timu yao tena ikiwa katika mji huu na kusema
watashilikiana bega kwa bega kuhakikisha timu inapata pointi 3 kwenye
mchezo huo.
Kesho jioni Young Africans itafanya mazoezi
katika uwanja wa kaitaba yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo
wa siku ya jumamosi.
Wachezaji waliofanya mazoezi leo jioni ni:
Walinda Mlango: Ally Mustapha 'Barthez', Deogratius Munishi 'Dida' na Yusuph Abdul
Walinzi : Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', na Kelvin Yondani
Viungo: Haruna Niyonzima, Athuman Idd 'Chuji', Frank Domayo, Nizar Khalfani, Mrisho Ngassa na Saimon Msuva
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Jerson Tegete, Hussein Javu, Said Bahanuzi na Abdallah Mguhi 'Messi'
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP
2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi
ya New B...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA