Mwaliko kwenye Kongamano la Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam 12/08/2013.
Kwa niaba ya Uongozi wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam, napenda kuwakaribisha watanzania wote wenye mapenzi mema
kwenye kongamano la kujadili mchango wa rasilimali zetu kwa maendeleo
ya taifa letu. Kongamano hilo litafanyika tarehe 8 Desemba 2013 ndani
ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia saa 7.30
mchana hadi saa 12 jioni. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV
na Radio one.
Mada kuu ya
kongamano hilo ni, “Mchango wa Rasilimali zetu katika maendeleo ya Taifa
na Nafasi ya Mtanzania Kumiliki Rasilimali hizo”.
Tunapenda
kuchukua fursa hii kwa heshima kubwa kuwaomba wote wenye uchungu na
rasilimali zetu na wadau wote wenye uelewa mpana kuhusiana na masuala ya
usimamizi wa rasilimali mfike ukumbini siku hiyo ili muwe miongoni mwa
watanzania wenye nafasi kubwa ya kutoa mchango wao katika kutoa elimu
kwa watanzania juu ya nafasi yao katika kumiliki rasilimali zetu na
mchango wake kwa maendeleo ya taifa letu.
Miongoni mwa
wazungumzaji siku hiyo ni pamoja na maprofesa waliobobea katika
usimamizi wa rasilimali, wazungumzaji wengine waalikwa ni pamoja na
Mheshimiwa John Mnyika (Waziri kivuli wa Nishati na Madini), Dkt
Reginald Mengi (Mwenyekiti wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania), na
wadau katika sekta ya madini. Na Mgeni Rasmi atakayefunga kongamano hilo
ni Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushiriki wenu kwenye kongamano hili.
Karibuni nyote:
Mr. Faraja Kristomus
(Katibu – UDASA)
0787525396 / 0717086135
Kwa maoni kuhusu mada husika tuandikie: kongamanoudasa@gmail.com
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA