MKWASA - NIYONZIMA, CANNAVARO HAWAKUPIGANA
Benchi la Ufundi la klabu ya Young Africans
limesikitishwa na taarifa zilizoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari
kwamba wachezaji wa Young Africans kiungo Haruna Niyonzima na nahodha
Nadir Haroub "Cannavaro" walipigana katika mchezo dhidi ya Coastal Union
siku ya jumatano jijini Tanga kuwa hazina ukweli wowote bali ni katika
kutaka kuharibu twasira ya timu.
Akiongea na mtandao rasmi wa klabu www.youngafricans.co.tz ,
kocha msaidizi wa Young Africans Charles Boniface Mkwasa amesema wao
benchi la ufundi wameshangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona na
kuzisoma leo na kusisitiza walioandika wamefanya hivyo kwa ajili ya
maslahi yao tu.
Kila mtu alikuwepo uwanjani na aliweza kushuhudia
mchezo huo, hakuna aliyeona Cannavaro na Niyonzima wakipigana katika
kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, nashikwa wasi wasi na waandishi
waliokuwepo uwanjani kama walikua makini kufuatilia mchezo na kuandika
kitu tofauti na walichokiona.
"Sheria za soka zipo wazi, mchezaji
au wachezaji wapigana ndani ya uwanja mwamuzi anawatoa nje ya uwanja kwa
kuwapa kadi nyekundu, sasa tumeshangazwa na taarifa hizo zilioripotiwa
leo kuwa kuwa kuna wachezaji wetu walipigana ili wachezaji wote
walicheza kwa dakika 90 "alisema Mkwasa.
Nadhani imefika wakati
tuisaidie jamii kuelewa uhalisia wa jambo husika liliotokea, kwani
kuandika tofauti na kilichotokea kunasababisha jamii kuamini/kuelewa
jambo ambalo silo lililotokea.
Katika
mchezo wowote wachezaji kuelekezana/kukumbushana majukumu ni jambo la
kawaida na ndicho kilichotokea katika mchezo dhidi ya Coastal kati ya Cananavaro na Yondani na Niyonzima na Cannavaro na si kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.
"Hata mara
baada ya mchezo wachezaji wote walikuwa pamoja na kupeana pole kutokana
na ugumu wa mechi, kisha wote kuondoka kuelekea hotelini kupumzika, na
sisi kama viongozi hatujaona wachezaji kutofautiana kitu chochote hata
kufikia hatua ya kusuruhishwa kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo
vya habari "aliongeza Mkwasa .
Kuhusu maandalizi ya mchezo wa
jumapili Mkwasa amesema vijana wake leo wamefanya mazoezi asubuhi
kujiandaa na mchezo huo, na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kwani
Hamis Kiiza, Hassana Dilunga waliokuwa wagonjwa wameshaungana wenzao
kambini na Athuman Idd "Chuji" aliyekua amesimamishwa kurejeshwa
kundini.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA