Jan 27, 2014

Young Killer sasa ni muziki na shule, aanza rasmi masomo ya IT



Young Killer sasa ni muziki na shule, aanza rasmi masomo ya ITYoung Killer Msodoki, rapper mwenye umri mdogo aliyefanikiwa kuiteka Tanzania na hata kuifikisha sauti yake Marekani na kumpata shabiki ‘mzungu’ aliyejirekodi na kuweka ujumbe wake youtube kueleza jinsi anavyomkubali, sasa amefanikiwa kuishi ndoto yake ya kujiendeleza kimasomo.

Rapper huyo ambaye hivi karibuni alieleza wazi kuwa anahitaji msaada wa kifedha ili aweze kurudi shule, ameingia rasmi darasani kusomea Information Technology (IT).

“Am..back…class…”, ameandika Instagram na kupost picha inayomuonesha akiwa anasoma huku ana headphone shingoni (Muziki na Shule).

Young Killer amejiunga na chuo kiitwacho ‘Green Pasture’ wiki mbili zilizopita. Kuanzia katikati ya mwaka jana, Young Killer alianza kuweka wazi wazo lake la kutaka kurudi shule na aliwahi kutaja masomo ya IT kuwa ndiyo ambayo angependa kusomea.

Tunamtakia kila la kheri kwa hatua nzuri aliyoipiga.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA