Feb 24, 2014

AZAM YAOMBA RADHI KWA MASHABIKI WAKE KUTOKANA NA MATOKEO MABAYA WALIYOYAPATA

 

Uongozi wa Azam FC kwa niaba ya benchi la ufundi na wachezaji, tunaomba radhi kwa mashabiki wetu mnaotupenda na kutuunga mkono kwa matokeo mabovu na mpira mbovu tuliouonesha jana.

Mpira na matokeo yale havilingani na uwekezaji, huduma na matarajio ya wamiliki, wapenzi na mashabiki wa kweli wa Azam FC, Lengo la uongozi mwaka huu ilikuwa ni kucheza angalau raundi ya makundi ya mashindano ya kombe la shirikisho na pia kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania. Kwa matokeo ya Beira Mozambique na jana Chamazi, ni dhahiri ndoto za mashindano ya kimataifa zimekufa kabisa huku ile ya kutwaa ubingwa wa Tannzania ikiwa rehani.

Azam FC inawaomba radhi watu wote mlioumizwa na matokeo haya na kama taasisi tutakaa chini, tutajiuliza, tutajitazama, tutajipanga na kuweka mikakati ya usajili makini ili kuanzia msimu ujao tusiwe na hali ya kizungumkuti kama hii

Tunaomba mashabiki wetu muendelee kutuunga mkono hasa wakati huu tunapoelekea kwenye mechi ngumu ya ligi kuu dhidi ya Ashanti United jumatano hii
Jumatatu Njema
Imetolewa na Utawala


0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA