Mar 4, 2014

Nikki wa Pili asema 'Weusi' imemsimamisha kazi Lord Eyez, Msikilize hapa

Nikki wa Pili asema

Msemaji wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa rapper Lord Eyez amesimishwa kazi katika kampuni hiyo na kwamba kwa sasa sio ‘member’.

 “Kitu ambacho naweza kusema kutoka Weusi ni kwamba Lord Eyez tumemsimamisha kazi kikampuni.” Amesema Nikki wa Pili na kusisitiza kuwa hajafukuzwa kazi bali amesimamishwa.

Hata hivyo, Nikki wa Pili hakuwa tayari kuweka wazi moja kwa moja sababu zilizopelekea Weusi kumsimamisha kazi rapper huyo.

“Hizo ni confidential, ni issue za kampuni hatuwezi kuziweka wazi lakini Lord Eyez tumemsimamisha kazi hiyo ndio taarifa ambayo tunaitoa kwa media.” Nikki wa Pili ameeleza.

Ameongeza kuwa kwa sasa matukio yote yanayotokea kwa upande wa Lord Eyez yatakuwa yanamhusu yeye binafsi na hayatakuwa na uhusiano wowote na kampuni.

Hii inamaanisha hivi sasa Weusi inaundwa na Joh Makini, Nikki wa Pili, G-Nako na Bonta.

Uamuzi huo wa Weusi umekuja wakati ambapo kumekuwa na taarifa kuwa Lord Eyez alikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi Jumamosi, huko Arusha na baadhi ya picha za tukio hilo kuonekana. Taarifa hizo zimedai kuwa anatuhumiwa kwa wizi wa laptop aina ya 'Dell'.

Mwaka juzi, Lord Eyez alikamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za wizi wa Power Window za gari la Ommy Dimpoz, lakini Ommy alitangaza kumsamehe msanii huyo.

Weusi walichukua dhamana ya kumtetea na kumuwekea mwanasheria huku wakifanya mikutano na waandishi wa habari ili kuitengeneza image ya kampuni hiyo ambayo ilikuwa imewekewa alama na tuhuma za Lord Eyez ambaye ni member wa kundi la Nako 2 Nako. 


0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA