Feb 10, 2014

Shabiki wa Arsenal amuua mtani wake wa Liverpool



Shabiki wa Arsenal amuua mtani wake wa Liverpool nchini Kenya kutokana na hasira....baada ya kichapo cha Jumamosi....Liverpool 5-1 Arsenal 


Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo wawili hao walianza malumbano baada ya mechi kati ya vilabu hivyo kumalizika hapo Jumamosi. 

Wawili hao walikua katika baa moja iliyojaa mashabiki wa timu hizo mbili. 

Shabiki wa Arsenal anayefanya kazi ya Boda Boda alijawa na hasira baada ya timu yake kukemewa na shabiki wa Liverpool kiasi cha kumdunga mwenzake kisu mara kadhaa, kabla ya kutoweka. 

Watu waliokua karibu na eneo la tukio hilo walimsaidia mwathiriwa aliyetambuliwa kama Anthony Muteithia na kumpeleka katika hospitali kuu ya Meru ambapo alifariki dunia wakati akipokea matibabu.
Mkuu wa polisi eneo la Meru Tom Odero amesema wanamsaka shabiki huyo wa Arsenal ambaye amekwenda mafichoni.

Hapo Disemba mwaka jana shabiki wa klabu ya Manchester United nchini Kenya kwa jina Jimmy Macharia alijiua baada ya klabu hiyo kuendelea kuorodhesha matokeo mabaya.

Na mnamo mwaka 2012 Suleiman Alfonso Omondi shabiki wa Arsenal alijitia kitanzi baada ya timu hiyo kushindwa kwenye mechi. Ligi ya Premia nchini Uingereza huvutia ushabiki mkubwa nchini Kenya na Afrika Mashariki kwa ujumla.

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA