Uongozi wa Young Africans unawaomba wapenzi, wanachama na wadau wa
soka kuacha kusoma habari za blog ya Bin Zubeiry kutokana na kuandika
taarifa zisizokuwa na ukweli huku lengo lake kubwa likiwa ni kuhakikisha
timu ya Young Africans inafanya vibaya kwenye michezo yake na kuwavunja
moyo viongozi wake pamoja na wachezaji.
Akiongea na mtandao rasmi wa klabu Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano Abdallah Binkleb amesema uongozi wao
umemvumilia kwa muda mrefu juu ya habari zake za kutaka kuwavunja nguvu
na kuisusa timu ili ibakie katika hali mbaya zaidi lakini kwa saaa
umechoka na hatua za kisheria zinafuata.
"Kuelekea mchezo
wa jumapili Waziri wa mambo ya nje anasisitiza timu ikafanye vizuri
kwani inabeba bendera ya nchi, balozi anashiriki maandalizi ya kupokea
timu mara itakapofika Misri lakini muandiishi huyu kazi yake imebakia
kuandika uongo juu ya Yanga lengo lake ni kuondoa morali kwa wachezaji
alisema" Bin Kleb
Hakuna asiyetambua kwamba Al Ahly walipokua
jijini Dar es salaam alikuwa nao bega kwa bega Uwanja wa Taifa siku moja
kabla ya mchezo wakati wakifanya mazoezi, wakati waandishi wenzake
wakionysesha uzalendo na kuandika habari zenye mlengo wa kuisaidia timu
ya Yanga kufanya vizuri.
Inafahamika
kilichomuondoa Habari Cooperation na kuamua kuendesha blog ambayo
halipii chochote kwa mwezi wala kwa mwaka zaidi ya kupata pesa za
matangazo kutoka wadhamini wanaomdhamini kwa kulipia matangazo yao kwake
na kupata idadi kubwa ya wasomaji kwa kuandika habari za Yanga.
Tunaomba
aachane na habari za Yanga kwenye blog yake vinginevyo taratibu
zinafanyika kuweza kuushtaki mtandao huo ambao umekosa weledi kwa
kuandika taarifa za kupotosha muda wote, huku klabu ya Yanga ikiambulia
kuchafuliwa na yeye kujipatia pesa kwa habari hizo.
Ni jambo la
kushangaza katika dunia ya sasa ya karne ya Sayansi na Teknlojia
mwandishi wa habari kuandika habari zisizokua na ukweli jambo ambalo
linapelekea wapenzi, wadau na wachama kushindwa kuelewa ukweli ni upi na
kuwapa kazi uongozi kujibu hoja zao.
Taarifa kwamba Uongozi
ulitoa posho ya laki moja sio kweli, hiyo ni pesa iliyotolewa mfukoni na
mmoja wa viongozi wa Young Africans kufuatia furaha ya ushindi mara tu
baada ya kumalizika kwa mchezo, Kamati ya mashindano ilikua na zawadi
nyingine ya ushindi huo ambayo wachezaji wameshakabidhiwa.
Tumewekeza
kwa zaidi ya miaka miwili sasa, tumesajili wachezaji wazuri, wanapata
huduma nzuri ikiwemo timu kuweka kambi nchini Uturuki mara mbili na
mazingira ya michezo ya ligi kuu ikiboreshwa kwa asilimia 100, mishahara
wachezaji wanapata kila mwisho wa mwezi hayo ni mabadiliko kiungozi na
kuelekea kwenye mafanikio katika mchezo wa mpira wa miguu.
Suala
la Ahadi/Zawadi ni nje ya mkataba kati ya wachezai na viongozi, klabu
imekua na utamaduni wa kutoa Bonus kulingana na ushindi unaopatikana, au
mara timu inapotoka sare hivyo ni vyema angeweza kuuliza uongozi kabla
ya kuandika vitu asivyovijua.
Aliandika kuhusu uwezo wa Kocha
Hans takribani kwa mwezi mzima pasipo kujua taaluma yake, Hans ni
miongoni mwa makocha wachache wenye Cheti cha Ualimu wa Mpira Miguu
barani Afrika CAF chenye Daraja A ambacho hutolewa kwa kocha aliyepata
mafanikio tu na si kwa kusomea darasani kama ilvyo kwa madaraja
mengine.
Mkataba wa SGM ulikuwa ni wa dolla 55,000 ambapo walitoa
Advance ya dolla 20,000 kisha ikabakia dolla 35,000 ambazo walipaswa
kuilipa Yangakabla ya kuanza kwa mchezo wenyewe, lakini SGM walitoa
sababu kuwa ofisa wao aliyekua anakuja na pesa hizo amezuiliwa Cairo
Airport na kuomba wapewe link waonyeshe mpira na watamalizia malipo hayo
baada ya mechi, Uongozi wa Yanga ulikuwa makini na kuwakatalia kuwapa
link mpaka wamalizie pesa iliyobakia kwani endapo wangepata hiyo link
basi ingekuwa vigumu kumalizia malipo baada ya mchezo kumalizika.
Taarifa
hizo zote na nyingine amekua akiandika bila kuwauliza viongozi wa Yanga
kupata uhakika jambo linalopelekea kuamini kuwa anatumika na baadhi ya
taasisi kuisakama Yanga ionekana haipo makini na kuonekana viongozi wake
hawapo makini jambo ambalo sio kweli.
Tunatambua ana masilahi na
upande gani, na timu gani ila kwa sasa tunaomba aachane na klabu ya
Yanga aandike taarifa za upande unaotumia kuhakisha anaiharibia Yanga,
akumbuke Yanga ilikuwepo na itaendelea kuwepo, wengine wanakuja na
kuondoka kama upepo.
Mwisho tunaomba aachane na taarifa za Yanga
aendelee kuandika habari za wafadhili wake wanaomsadia kwani hata wao
habari ni nzuri, habari za Yanga ziwe nzuri au mbaya zitaendelea
kuandikwa na waandishi wenye weledi na wanaoheshimu taasisi
zinawapowaptia habari.
Mungu Ibariki Young Africans Mungu Ibariki Tanzania.
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP
2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi
ya New B...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA