Helena Costa kuwa mwanamke wa kwanza kufundisha soka la kulipwa Ufaransa
Helena Costa kocha mpya wa timu ya Clermont ya Ufaransa
Helena Costa raia wa Ureno atakuwa mwanamke wa kwanza kuwa kocha wa timu
ya kulipwa ya wanaume nchini Ufaransa baada ya kutangazwa na timu ya
Clermont Foot 63 kuwa kocha wake mkuu, Jumatano.
Helena Costa mwenye umri wa miaka 36 kwa sasa ni meneja wa timu ya taifa
ya Iran ya wanawake, akiwa amewahi pia kusaidia usajili kwa timu ya
Celtic na kuwa meneja wa timu ya wanawake ya Qatar.
Uteuzi wake utasaidia timu ya Clermont Foot 63 kuingia katika kipindi kipya", amesema Clermont.
Clermont inashika nafasi ya 14 katika msimamo wa Ligue 2 nchini Ufaransa ikibakia michezo miwili kukamilisha msimu wa ligi hiyo.
Clermont itawategemea wachezaji 17 ambao kwa sasa bado wana mikataba na itawaongeza wachezaji chipukizi kutoka timu hiyo.
Olivier Chavanon, amekuwa na uzoefu mkubwa na uelewa wake wa kina wa timu hiyo utasaidia kuwa karibu zaidi mchezoni.
Utambulisho wa meneja mpya wa timu ya Clermont utafanyika Clermont-Ferrand mwisho mwa msimu wa 2013/2014.
chanzo na BBC
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA