May 7, 2014

HIVI NDIVYO MAZISHI YA SHEKH ILUNGA HASSAN KAPUNGU KATIKA MAKABURI YA MWINYI MKUU MAGOMENI


Hapa ndipo alipozikwa Shekh ILUNGA HASSAN KAPUNGU hapo jana katika makaburi ya Mwinyimkuu yaliyopo Magomeni

 
Vijana wakiwa juu ya mti ili nao waweze kushuhudia mazishi yanavyokwenda ingawaje walikuwa mbali na tukio kutokana na wingi wa watu waliofurika kwenye eneo makaburi ya Mwinyimkuu 








Shekh Kishki akichukua koleo lenye mchanga ili aweze shiriki mazishi
 
Katika ni picha ya Shekh Ilunga Hassan Kapungu akiwa katika zama za uhai wake
 
Maalim Seif akiwa pamoja na Profesa Lipumba wakishiriki mazishi ya Shekh Ilunga

Mazishi ya Shekh Ilunga yalikuwa ni ya kihistoria na ya pekee kwani kutokana na wingi wa watu waliohudhuria kwenye eneo hilo,ilalazimika watu kufukia kaburi kwa mikono ili kila mmoja apate kushiriki mazishi hayo kwa kufukia kaburi.


Shekh Ilunga atakumbukwa kwa mawaidha yake yenye kujenga pamoja kuwaamsha waislam waliokuwa wamezama kwenye dimbwi la dhuma na kufanywa kuwa takaba duni.Shekh Ilunga alipelekwa India kwa mara ya kwanza kwa ajili ya matibabu kisha kurejea nchini akiwa na afya iliyoanza kutengemaa.


Baada ya muda hali yake ikawa si nzuri hivyo akarejeshwa tena nchini India kwa ajili ya kupata matibabu.Alilerejea nchini katika siku za hivi karibuni lakinia afya yake ikawa bado sio nzuri.Inasemekana alikuwa akipoteza fahamu kwa muda kisha fahamu kurejea na ndipo hapo juzi usiku wa saa tano alipofariki 

kwa habari zaidi bofya hapa

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA