May 12, 2014

MANJI AUNGURUMA

  Mwenyekiti wa Young Africans Bw Yusuf Manji akiongea na wanachama, wazee na waandishi wa habari leo makuu ya klabu ya Yanga

Mwenyekiti wa Young Africans Bw Yusuf Manji amesema kuondoka kwa wachezaji wao wawili Didier Kavumbagu na Frank Domayo sio mwisho wa timu ya Yanga, kwani uongozi wake unaendelea na mipango ya kuhakikisha inasajli wachezaji wengine wazuri ambao wataisadia timu kwenye msimu ujao kwa kufuata maelekezo ya Benchi la Ufundi.

Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu leo, Manji amesema yameongelewa mengi sana kwa kipindi cha mwezi mmoja ambao hakuwepo nchini kwa ajili ya kazi zake binafsi lakini sasa amerejea na maandalizi ya msimu ujao yameshaanza.

Kuondoka kwa Kavumbagu ni kutokana na kuchelewa kwa majibu ya TFF juu ya idadi ya wachezaji wageni kwa msimu mpya, huku Domayo ambae tangu mwaka jana aliombwa kuongeza mkataba alikua akisema anamsubiria mjomba wake ndipo aweze kufanya hivyo.

Pamoja na kuondoka kwa wachezaji hao bado kwa kushirikiana na kocha Hans watahakikisha Yanga inaendelea kutisha msimu ujao na kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa, Hans aliahidi kuleta wachezaji wazuri watakaoisaidia Yanga siku alipokua akiiongea na waandishi wa habari kuwaaga.

Aidha Manji amelifuta rasmi tawi la Tandale kutokana na kuwa na chanzo cha vurugu na migogoro ndani ya klabu, pia amewafuta uanachama wanachama sita ambao walikiuka katiba ya Yanga kwa kwenda kuongea na waandishi na HABARI bila ya Idhini ya uongozi huku pia wakishindwa kulipia ada zao za uanachama kwa zaidi ya miezi sita, waliofutwa uanachama ni:

1. Ally Kamtande, 2. Isiaka Dude, 3. Hamisi Matandula, 4.Waziri Jitu Ramadhani, 5.Mohamed Kigali Ndimba , 6. Selaman Hassan Migali 

Mkutano mkuu wa mabadiliko ya katiba utafanyika terehe mosi Juni, 2014 katika Ukumbi wa Oysterbay Police Mess na wanachama wote wanaombwa kulipia ada zao ili waweze kuhuhudhira mkutano huo wakiwa hai. 

Suala la ujenzi wa Uwanja wa Kisasa eneo la Jangwani bado lipo pale pale, kikubwa kinachosubirwa ni majibu ya serikali juu ya maombi ya eneo la ziada, kwani Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam alisema suala hilo lipo ukingoni na mda si mrefu.
  

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA