Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu
amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu
wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria
wataachiliwa huru.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA