Pombe yenye sumu yawaua 76 Kenya
Washukiwa waliouza pombe hiyo wameripotiwa kukamatwa
Watu wawili wamekamatwa nchini Kenya kuhusiana na mkasa wa watu zaidi ya
70 kufariki kutokana na kunywa pombe iliyokuwa imetiwa sumu.
Vifo hivyo vimetokea katika muda wa saa 48 baada ya walevi kuanza kulewa siku ya Jumapili na Jumatatu asubuhi.
Pombe hiyo iliyopewa jina la 'Countryman', inasemekana iliwekwa sumu
aina ya Methanol na kusababisha baadhi ya waliokuwa wamekwenda kuibugia
kufariki huku wengine wakisalia hali mahututi na wengine kupoteza uwezo
wao wa kuona.
Madaktari wanafanya kila wawezalo kujaribu kuokoa baadhi ya waathiriwa ambao wamelazwa hospitalini.
Vifo hivyo vilianza kutokea mapema wiki hii katika mkoa wa kati na katika eneo la Mashariki mwa Kenya.
Inaarifiwa wengine wengi wamelazwa hospitalini baada ya kubugia pombe hiyo.
Idadi ya vifo ilianza kuongezeka huku watu wengine 14 wakifariki katika
jimbo la Embu Mashariki mwa nchi , wengine wanne wakifariki katika jimbo
la Makueni. Watu 75 wamelazwa hospitalini katika jimbo hilo wengine
watatu wakiripotiwa kupoteza uwezo wao wa kuona.
Kwa sasa wataalamu wanafanyia utafiti kinywaji hicho pamoja na mkojo
kutoka kwa wagonjwa kubaini kilichowekwa ndani ya pombe hiyo.
Matokeo yanatarajiwa katika siku mbili zijazo.
Hadi sasa watu 76 wanasemekana kufariki kutokana na pombe hiyo katika maneo mbali mbali ya nchi.
chanzo na BBC
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA