Aug 22, 2014

Babu Tale ajibu tuhuma za Diamond kufanya biashara ya 'Unga'

Babu Tale ajibu tuhuma za Diamond kufanya biashara ya

Meneja wa Diamond, Babu Tale amekanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Amani la leo (August 21) zilizomtuhumu msanii huyo kuwa anajihusisha na dawa za kulevya.

Babu Tale ameongea na mtandao wa Bongo5 na kuonesha kuchukizwa na taarifa hizo na kueleza jinsi ambavyo msani huyo huingiza pesa nyingi kwa kutumia muziki wake.

Haya ni majibu ya Babu Tale:

“Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.

“We get more money from music, sio kwenye madawa ya kulevya, hatufanyi hizo biashara na kama wanahisi sisi tunafanya tunawaruhusu watufanyie investigation hata kwa muda wa miaka kumi ina maana tunavyopita pale airport hawana vifaa vya kutuchunguza? Ipo wazi hata Global walishindwa kufanya kazi na sisi kwa sababu sisi ni wakubwa. Sasa leo hii tunauza madawa ya kulevya kwa sababu tunakomaa kwenye bei zetu. 

“September tunafanya show kubwa ya Unplugged na msanii wa kwanza hapa kufanya ile show ni Diamond na ile show hawalipi hela ya kis**e, wataendelea kuona watu wanauza madawa ya kulevya, hakuna msanii wa Tanzania anayefanya show kwa walau dola elfu 10,000 ni Diamond peke yake wengine ni dola  2000, 2500  elfu 3,000 mwisho. Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola elfu 15,000.”

Chanzo: Bongo5

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA