Mwneyekiti wa Yanga SC Bw Yusuf Manji (kulia) akiongea na waandishi wa
habari leo makao makuu ya klabu juu ya sakata la Okwi, kushoto ni makamu
mwenyekiti Bw Clement Sanga
Klabu ya Young Africans imemshitaki mchezaji Emmanuel Okwi kwa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho
la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa
kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka
miwili.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga mitaa
ya Twiga/Jangwani, mwenyekiti wa Yanga Bw Yusuf Manji amesema
wameshangazwa na kitendo hicho kilichofanywa na viongozi wa Simba ,
wakala wake na mchezaji mwenyewe.
"Emmanuel Okwi awali
tulishapeleka malalamiko TFF na kuwapa nakala CAF na FIFA juu ya kufanya
mazungumzo na timu ya Wadi Degla FC ya nchini Misri na kufikia klabu
hiyo kutuma ofa ya kutaka kumnunua bila kuwasiliana na uongozi wetu"
alisema Yusuf.
Ikiwa hilo tunasubiria majibu kutoka TFF jana
mchezaji huyo amesaini mkataba mwingine, hii inaonyesha ni jinsi gani
mchezaji huyu kuna watu walikua wanamrubuni,kwa kusaini mkataba mwingine
kitu ambacho amekiuka sheria za FIFA za usajili.
Baada ya kuona
jana amesaini mkataba na Simba, Yanga tulichokifanya leo ni kuandika
barua nyingine TFF juu ya suala hilo na kuomba kulipwa fidia ya US
Dollar 500,000 (sawa na TZS 800,000,000/=) kutoka kwa klabu ya Simba,
wakala wake na mchezaji mwenyewe aliongeza "Manji"
Aidha
uongozi wa Yanga umeiomba TFF kuwa imelipatia ufumbuzi suala hilo ndani
ya siku saba, na kama siku saba zikikpita basi uongozi wa Yanga
utakwenda moja kwa moja FIFA na ikishindakana mahakama ya soka CAS.
Lengo
sio kuikomoa timu ya Simba, bali tunachotaka ni sheria ifuatwe, Okwi
alikua ameitumikia klabu ya Ynaga kwa kipindi cha miezi sita tu, na kuwa
amebakiza mkataba wa miaka miwili mpaka msimu mwishoni mwa msimu wa
2015/2016.
Mchezaji anayekutwa na kosa la kusaini sehem mbili
adhabu yake ni kufungiwa kucheza soka kuanzia mwaka mmoja na kuendelea
huku klabu husika ikifungiwa kusajili kuanzia miaka mwili na kuendela na
kushushwa daraja au adhabu zote kwa pamoja.
BONDE FC NI MABINGWA WAPYA WA BEIRA YOUTH CUP 2012
-
Timu ya Bonde fc jana iliibuka kuwa mabingwa wapya wa BEIRA YOUTH CUP
2012 ubingwa huo umepatikana baada ya kuibuka na ushindi wa gili 5-4 dhidi
ya New B...
12 years ago
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA