Aug 13, 2014

HII SASA NI HATARI KAMPUNI MOJA NCHI JAPANI YATENGENEZA MIDOLI YA MAPENZI 'real Love Dolls', TAZAMA VIDEO HAPA

Video: Kampuni ya Japan yaingiza sokoni midoli ya mapenzi

Kampuni ya Japan inayojulikana kama Orient Industry imeingiza sokoni midoli yenye umbo na sura ya wasichana wenye mvuto wa aina mbalimbali, maalum kwa wanaume kufanya nayo mapenzi kama wasichana halisi (Real Love Dolls).

Kampuni hiyo ilianza kutengeneza midoli hiyo tangu mwaka 1977 na imekuwa ikiiboresha kila wakati ili kuipa uhalisia katika suala la mapenzi, na hadi sasa meweza kuingiza sokoni midoli ya aina tatu maalum kwa ajili ya tendo hilo.
 
Kwa mujibu wa kampuni hiyo, mdoli mmoja unauzwa $ 2.7 na ukiitazama bila kuigusa ni vigumu kuitofautisha na msichana/ mwanamke halisi mwenye mvuto kwa kuwa mtumiaji anaweza kuigeuza katika position aitakayo.

Katika aina hizo tatu, kampuni hiyo imeeleza kuwa aina moja imetengenezwa katika hali ambayo itawasaidia hata wanaume ambao ni walemavu wa viungo vya mwili.

Tayari kampuni hiyo imeanza kusambaza matangazo ya bidhaa hiyo kwa wateja wao huku ikipost videos kwenye YouTube kuhusu jinsi ya kuitumia midoli hiyo.


http://www.timesfm.co.tz

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA