Hatimae diwani wa Makumbusho mh Ally Haroub amejitosa katika kusaidia ukarabati wa uwanja wa Bonde Fc.diwani alifikia hatua hiyo baada ya kutembelea uwanja na kuona jinsi ulivyoharibika.
Alipoalikwa katika kikao cha
wanakamati ya kukarabati uwanja alifika na ndipo alipowahaidi kuwa
atashuhurukia uwanja kwani suala hilo lipo ndani ya uwezo wake na kwa
kushirikiana na kamati ya uwanja anahuhakika wa kuifanya kazi hiyo bila
tatizo.
Pia katika kikao hicho kamati ndogo ya
kusimamia ukarabati iliundwa na diwani akiwa mmoja wa wajumbe wa kamati
hiyo akiwataja wajumbe wa katimati hiyo mratibu wa uwanja wa Bonde Fc
ndugu Rashid Maulid Banda alisema kamati inaundwa na watu watano
Nae mwenyekiti wa kamati ya muda
iliyoundwa ndugu Omary Maloki amehaidi atahakikisha kamati yake inafanya
kila linalowezekana ili kufanikisha matengenezo ya uwanja kwa
kuwatafuta wafadhili mbali mbali ili kufikia malego.
- MWENYEKITI OMARY MALOKI
- KATIBU RAMADHANI FARAHANI
- MJUMBE EMANUEL I ISHENGOMA
- NJUMBE MASOUD HEMED
- MJUMBE MH: ALLY HAROUB
- MJUMBE RASHIDI BANDA
Kutokana na hualibifu huo umesababisha
timu kuwa na wakati mgumu kutokana wa kukosa uwanja wa kufanyia mazoezi
hali iliyopelekea timu kuomba uwanja katika shule ya msingi Tuliani
Magomeni jambo ambalo ni hatari kwa wachezaji wa under 14 kwani
inawaladhimu kuvuka barabara.
Na hata eneo lenyewe linalotumika kwa mazoezi ni dogo hivyo kusababisha timu kukosa muda wa kucheza full game kwani kila siku wanacheza open space hali ambayo imekuwa ikiwafanya vijana kupata sana tabu katika mechi kutokana na kuzoea kucheza katika stahili hii.
Pia hali hii imepelekea wachezaji wengi
kukimbia na kwenda kufanya mazoezi katika viwanja vingine na wengine
kufanya mazoezi siku mojamoja.
habari na mtandao wa bonde fc www.bondefootballclub.blogspot.com
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA