May 30, 2012

HIVI NDIO UWANJA WA BONDE FOOTBALL CLUB ULIVYOHARIBIKA

Hii ndio hali ilivyokatika uwanja wa timu ya Bonde Fc ya Mwananyamala baada ya kuharibikwa kabisa na mvua zilizonyesha mapema mwaka huu.


Hivi ndio hali ilivyo katika uwanja wa Bonde Fc baada ya kuhalibiwa na mafuriko yaliyotokea mwanzoni mwa mwakaka huu.

Juzi timu ya Bongo Yetu ilipata nafasi ya kutembelea uwanja wa timu hiyo uliopo katika mipaka ya
Mwananyamala na Magomeni nakujionea jinsi ulivyoharibiwa na mvua hizo.

Kutokana na uhalibifu huo umesababisha timu hiyo kukosa sehemu ya uhakika ya kufanyia mazoezi na kulazimika kufanya mazoezi katika uwanja mdogo uliopo katika shule ya msingi Tuliani Magomeni

Pia amesema kutokana na hali hiyo amesema wachezaji wote wa timu hiyo wa under 14 wapekuwa hawatokei kabisa mazoezini kutokana na wengi kushindwa kuvuka barabara kuelekea Magomeni  kufanya mazoezi   

Hata napo kocha wa timu hiyo ndugu Issa Joseph amesema pia katika uwanja waliokuwa wanautumia wa shule ya msingi Tuliani pia wamesimamishwa kuhutumia na hivyo kwa sasa wamesimamisha mazoezi ya timu hiyo kwa muda mpaka watakapopata ufumbuzi wa uwanja wao.

Hivyo basi wameomba kwa wale wote wenye kupenda soka la watoto kujitokeza kusaidia katika kuokoa uwanja wao na hatimae watoto wapate sehemu ya mazoezi na waweze kuendelea na mashindano mbalimbali kama kawaida yao

Pia kocha huyo wa timu ya Bonde Fc alisema timu yake pamoja na matatizo yote hayo bado inakabiliwa na michuano mingi na migumu.
Miongoni mwa michuano hiyo ni kombe la PRINCE CUP 2012 inayochezwa katika uwanja wa Mwalimu Nyerere Magomeni Mwembechai haya ni kwa timu yao ya (U21)  na Tarehe 6/6/2012 itacheza na Faru Dume ya Magomeni

Nayo timu yao ya U17 inakabiliwa na timu michuano ya VIJANA CUP inayoendelea katika uwanja wa Muslim Kinondoni na Jumapili hii  ya tarehe 3/06/2012 itacheza na ABBA FC ya Kinondoni

Na pia timu ya U21 inakabiliwa na michuano ya ligi ya inayochezwa katika uwanja wa BEIRA Kigogo na Jumamosi hii itakuwa na kibarua kingine dhidi ya NEW TEAM ya Ilala kwani katika mechi ya awali timu ya Bonde Fc iliibuka na ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Kigogo United.

Hiki ni kikosi cha Bonde Fc katika moja ya mechi zao katika uwanja wa BEIRA Kigogo
   

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA