May 30, 2012

KIJUE KIKOSI CHA UJERUMANI KITAKACHOCHUANA KWENYE MICHUANO YA EURO 2012

Jana kocha wa Ujerumani Joachim Löw's alitaja majina ya wachezaji 23 watakao iwakilisha nchi hiyo kwenye michuano ya UEFA EURO 2012 itakayoanza mapema mwezi ujao hata napo kocha huyo imemlazimu kupunguza wachezaji wake wanne ambao hapo awali walikupo katika kambi ya timu hiyo ambayo ilikuwa na jumla ya wachezaji 27

Wachezaji walioachwa na kocha Joachim Löw's ni pamoja na kiungo wa Borussia Dortmund Sven Bender wengine ni golikipa Marc-André ter Stegen  kijana wa miaka18 Julian Draxler nae pia ameachwa Cacau pia nae amechwa katika kikosi hicho 

Cacau amesema hajafurahishwa na kuachwa kwake katika kikosi cha Ujerumani ila anaunga mkono uwamuzi wa kuteua vijana katika timu hiyo 

Hata napo kikosi cha Ujerumani kinaonekana kujaza viungo wengi kuliko washambuliaji 

Pia kikosi cha Ujerumani kitacheza mechi moja ya kirafi nnchini Israel May 31 kabla ya kuanza michuano kwani Ujerumani itacheza na Ureno

Hiki ndio kikosi cha Ujerumani 2012

Magolikipa 
       Manuel Neuer (FC Bayern München), Tim Wiese (SV Werder Bremen), Ron-Robert Zieler (Hannover 96)

Mabeki 
  Holger Badstuber (FC Bayern München), Jérôme Boateng (FC Bayern München), Benedikt Höwedes (FC Schalke 04), Mats Hummels (Borussia Dortmund), Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund), Philipp Lahm (FC Bayern München), Per Mertesacker (Arsenal FC).

Viungo
         Lars Bender (Bayer 04 Leverkusen), Toni Kroos (FC Bayern München), Thomas Müller (FC Bayern München), Mesut Özil (Real Madrid CF), Sami Khedira (Real Madrid CF), Marco Reus (VfL Borussia Mönchengladbach), André Schürrle (Bayer 04 Leverkusen), Bastian Schweinsteiger (FC Bayern München), Mario Götze (Borussia Dortmund), İlkay Gündoğan (Borussia Dortmund).

Washambuliaje
   Miroslav Klose (S.S. Lazio), Mario Gomez (FC Bayern München), Lukas Podolski (1. FC Köln).

Picha chini ni  Cacau ambae ametemwa katika kikosi cha UjerumaniCacau among omissions from final Germany squad

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA