Oct 20, 2012

MKASA MZIMA WA KUTEKWA KWA SHEIKH FARIDI HUU HAPA


Amesema kuwa waliomchukuwa walijitambulisha kwake kuwa ni askari polisi na kumonesha vitambulisho huku wengine wawili wakiwa na silaha za mshingani hapo hapo wakamfunga macho yake kwa kutumia kitambaa ili asijue wapi anapelekwa walimchukua kwa gari na baadae kumuingiza katika nyumba asioijua kwa mahojiano bila ya kumfungua kitambaa hicho kwa muda wa siku tatu mfululizo.

Amesema kuwa watu hao waliomuhoji maswala mengi sana kuhusu tangu kuuanzishwa kwa jumuia ya uamsho na safari zake za kwenda omani na mpaka kumchukulia simu yake bila ya kumrejeshea pia wametaka kujua kuwa anauhusiano gani na rais shein na makamo wakwanza wa raisi maalim seif, wakati wanamuhoji walifika mpaka kupiga risasi chini ya miguu nyake ili kumtisha na kuweza kufikia lengo lao walilojipangia.


Amesema pia watu waliomchukuwa na baadhi ya waliokuwa wanamlinda hawezi kuwajua kutokana na kuwa walikuwa wamevaa soksi ndani ya nyuso zao nakubakisha macho tu,amsema kutokana tu na lafdhi zao ambazo walikuwa wanaongea inaonekana wazi kuwa wengi ni kutoka bara na wazanzibari ni kama wawili tu kutokana na sauti zao.

kuhusu suala lakupigiwa simu na mtu asiemjua amesena kuwa wao kama viongozi huwa mara nyingi wamekuwa wakipigiwa simu na watu wasiowajua na wamekuwa wakionanan nao bila ya matatizo hivyo basi kitendo cha kupigiwa simu siku hio na mtu asiemjua hakikumshituwwa kwani nikawaida kwao hususani aliemnigia alijitambulisha kama ni mwanafunzi wake wa mahad lmahfudh


Aidha amesema kuwa muda wote huo wa siku tatu hakuweza kula chochote katika chumba hicho kwani alikuwa hawaamini na badala yake alikuwa anakunywa maji kutoka bomba la mfereji lililokuwa chooni katika chumba hicho pia amesema wakati yupo ndani hakujua lolote linaloendelea huku nje isipokuwa amejua baada ya kutoka nje kwa kuambiwa na kila manaemkuta.


Aidha sheikh farid ameiomba serikali ya mapinduzi ya zanzibar kutumuia sheria na uadilifu kwa rai wake kinyume cha hivo watakuwa wanaimba tu katika nchi amani na utulivu usiokuwepo pia amewataka wazanzibar kuendelea kutetea maslahi ya nchi yao kama kawaida kwani kufanya hivo ni haki yao na yeye amewahakikishi ataendelea kuitetea zanzibar mpaka tone la mwisho la damu yae.
 
 Wazanzibar wakiwa wanakusanyika nyumbani kwa kiongozi wao Farid baada ya kuonekana  na mkono unaonekana ni wa Faridi akiwasalimia.

 
 Wazanzibar wakiwa wanasherekea mitaani  baada ya kuonekana shekhe Farid jana usiku.
 

Shekhe Faridi akiwa na waumini waliofika nyumbani kwake mara baada ya kuonekana jana usiku

Shekhe Faridi akiwa na mwanae mara baada ya kuwaachiwa toka mafichoni
 
Dua ikisomwa katika kumshuru Mungu baada ya shekhe Faridi kuonekana akiwa salama 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA