Oct 22, 2012

KESI INAYOWAKABILI VIONGOZI WA UAMSHO YA KHAIRISHWA MPAKA TAREHE 25/10/2012


Kesi ya Viongozi wa Uamsho inayowakabili imekhairishwa mpaka siku ya ALKHAMIS.
 Hakimu wa mahkama alitaja kesi inayowakabili viongozi hao ni
KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI NA KUSABABISHA VURUGU ZILIZOTOKEA MSUMBIJI MIEZI MIWILI NYUMA.

Kwa upande wa Mawakili wa walalamikaji walilamika sana kwa upande wa serikali kushindwa kuwapatia order paper ya washtakiwa hili linaonekanwa kuwa walikuwa hawajui wawape kesi gani.
 

Vile vile walilalamikia Jinsi Jeshi la polisi wanavovunja sheria kwa Kuwazuwia Mawakili hao kuonana na wateja wao ambao ni viongozi wa Uamsho ambacho nikinyume na sheria.
 

Vilevile Mawakili wa washitakiwa wameitaka mahakama kuondoa baadhi ya vipengele vya DHAMANA.
ikiwemo kuwepo kwa barua ya sheha kwani masheha wakifatwa hujifanya wanaviakao na hawataki kutoa.

Vile vile kuondoa kipengele cha kuwepo mdhamini moja ambae nimfanyakazi wa serikali.wanasheria hao wamesema haiwezekani ikawa serikali ndio inawashataki halafu lazima awepo mdhamini ambae anafanya kazi serikalini.
 

Baada ya makubaliano hayo Jaji ambae aliepangiwa kesi hiyo amesema kutokana na ugumu wa kesi hiyo ameomba kuihairisha mpaka siku ya ALHAMIS TAREHE 25.10,2012.
 
Hata napo baada ya kusomwa kesi hiyo hali imeonekana kuwa ya utulivu tofauti na ilivyotegemewa hapo hawali .
 
Ulinzi nao ulikuwa umeimalishwa kila kona hasa maeneo ya kukaribia mahakama
   
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA