Timu ya Young Africans Sports Club kesho siku ya jumamosi, itashuka
dimbani kucheza dhidi ya timu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi
kuu ya Vodacom Tanzania bara, mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans itaingia uwanjani kwa lengo la kusaka
pointi 3 muhimu ambazo zitapelekea kusogea katika nafasi tatu za juu,
na baadae kuweza kuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu
ya Vodacom 2012/2013.
Katika mchezo wa mwisho
dhidi ysa Toto Africans jini Mwanza, Young Africans iliibuka na ushindi
wa mabao 3-1, shukrani kwa mabao ya Mbuyu Twite, Didier Kavumbagu na
Jeryson Tegete.
Kocha mkuu wa Young Africans
Sports Club, mholanzi Ernie Brandts amesema vijana wake wote wako safi,
wanaendelea na mazoezi hivyo ana imani mchezaji yoyote atakayepangwa
atafanya vizuri katika mchezo huo.
Wachezaji
Kelvin Yondani na Said Bahanunzi ambao walikua majeruhi wanaendelea
vizuri na mazoezi, lakini kwa mujibu wa daktari wa timu Dr Suphian Juma
amesema wachezaji hao hawataweza kucheza mchezo wa kesho, kwani bado
hawajawa katika hali nzuri, ila wanaweza kuanza kucheza mchezo dhidi ya
Polisi Morogoro siku ya jumatano.
Viingilio vya mchezo ni:
VIP A 20,000/=
VIP B & C 15,000/=
Orange 8,000/=
Blue & Green 5,000/=
habari kwa hisani ya mtando wa yanga sport club
habari kwa hisani ya mtando wa yanga sport club
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA