YANGA YAENDELEA NA MAZOEZI LOYOLA, KUIVAA MGAMBO JKT JUMATANO TAIFA
Mabingwa mara mbili mfululizo wa kombe la Vilabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati (KAGAME),timu ya Yanga imeendelea na mazoezi leo
asubuhi katika Uwanja wa shule ya sekeondari Loyola tayari kwa ajli ya
kuikabili timu ya Mgambo JKT siku ya jumatano katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha wachezaji 20 na Benchi la Ufundi 7 kilirejea jana jioni
kutokea jijini Arusha ambapo katika mchezo wake dhidi ya timu ya JKT
Oljoro ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0, shukrani kwa bao
lililofungwa na mlinzi wa kati Mbuyu Twite dakika ya 53.
Wachezaji
wote wamefanya mazoezi asubuhi ya leo, kitu ambacho kocha Ernie
amefurahia kutokua na majeruhi hivyo anamini kikosi chake kiko tayari
kuivaa timu ya Mgambo JKTkatika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Kwa
matokeo hayo, Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania bara kwa pointi 20, ikiwa nyuma ya watani wa jadi
Simba wenye pointi 22 huku waoka mikate timu ya Azam FC ikiwa katika
nafasi ya nne, baada ya timu ya Coastal kushinda jana na kufikisha
pointi 19.
Kocha mkuu wa Yanga mholanzi Ernie Brandts amesema
anafurahishwa na mabadiliko ya kiuchezaji ya kikosi chake,kwani
wachezaji wake kwa sasa wanaonyesha kumuelewa anavyotaka wacheze,hivyo
anaamini mabadiliko mengi yataonekanakadri siku zinavyokwenda.
Brandts
ameongeza kwamba anapenda wachezaji wake wacheze pasi za haraka haraka
huku wakipanga mipango ya mashambulizi, na kwa sasa anaona wachezaji
wanaanza kumuelewa hali inayopelekea timu kuibuka na ushindi wa 4
mfululizo.
Katika michezo itakayochezwa siku ya jumatano, endapo
Yanga itashinda na Simba ikatoka sare basi Yanga itakamata usukani wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
Young Africans imebakisha
michezo michezo 3 kabla ya kumalizika kwa duru la mzunguko wa kwanza wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara
Chanzo na http://www.youngafricans.co.tz
0 Weka maoni yako hapa:
Post a Comment
COMMENT HAPA