Oct 23, 2012

CHAMA CHA WANANCHI CUF CHAZIDI JITUTUMUA

Juzi chama cha wananchi CUF kilifanya mkutano wa hadhara maeneo ya Buguruni mkutano ulioudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo makamu wa kwanza wa rais Zanzibar Maalim Seif sharifu Hamad.

Katika mkutano huo ambao chama cha wanannchi CUF kiliutumia kama sehemu ya kuwaeleza wanachama wapenzi na wananchi kwa ujumla nini kinachoendelea katika taifa hili na Zanzibar kwa hujumla kufuatia vurugu zinazoendela hapa nchini kwa sasa.

Pia katika mkutano huo wale waliokuwa wafuasi wa chama kipya cha siasa cha ADC alirudisha kadi na bendera za chama hicho na kuchukua kadi za CUF.

Pia inadaiwa aliekuwa katibu muenezi wa Chadema tawi la chuo kikuu Dodoma alirudisha kadi yake pamoja na kuvua gwanda kisha akapewa kadi mpya na kuvaa flana ya chama cha CUF mbele ya katibu mkuu wa CUF Maalim Seiff.

 sehemu ya umati uliojitokeza buguruni kwene mkutano wa CUF
Watu wakimsikiliza katibu mkuu wa chama cha CUF kwa makini hayupo pichani.

 Waliokuwa wanachama wa chama kipya cha ADC wakirudisha kadi na bendera za chama hicho na kuchukua kadi za CUF.
 Aliekuwa katibu muenezi wa Chadema chuo kikuu cha Dodoma akivua gwanda na kurudisha kadi ya Chadema na kujiunga na chama cha CUF hapa ikivishwa flana ya ya CUF.


0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA