Nov 1, 2012

YANGA, NJOROGE MAMBO SAFIKaimu Katibu Mkuu wa Young Africans Sports Club - Lawrence Mwalusako


Uongozi wa klabu ya Young Africans umemalizana na mchezaji wake wa zamani John Njoroge aliekua na madai yake ya kuvunjwa mkataba wake miaka miwili iliyopita, hali iliyompelekea Njoroge kuishtaki Yanga FIFA na jana jioni Uongozi umemalizana nae.

Akiongea na mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz  katibu mkuu wa Young Africans Lawrence Mwalusako amesema wamefikia mwisho juu ya suala na hilo ambapo jana jioni Njorogen alipokea pesa aliyokua akidai klabu ya Yanga.

Awali tulitangulia kumlipa tsh milioni 4 ambapo alitaka kumaliziwa pesa yake kwa pamoja, na jana klabu ya 

Young Africans ilimalizia kumlipa tshs milioni 14 kama alivyoelekeza na hivyo Yanga kuwa imemlipa jumla ya tshs milioni 17 alizokuwa anadai alisema 'Mwalusako' 

Mchezaji John Njoroge aliyejiunga na Young Africans akitokea Tusker FC ya Kenya amelipwa jumla ya tshs milioni 17 ambazo tayari amedhibitisha kuzipokea na kutuma kiambatanisho cha malipo FIFA 

John Njoroge alisajiliwa Young Africans mwaka 2008 kwa mkataba wa miaka miwili kabla ya kuongezewa tena mkataba wa mwingine ambao ulilkua na utata hatua iliyopelekea Njoroge kwenda kuishitaki Yanga FIFA. 

Kufuatia hatua hii Uongozi wa Young Africans unawashukuru wapenzi, washabiki na wanachama wake kwa kuwa na subira katika kipindi hiki ambacho uongozi ulikuwa unalishulikia suala hili. 


0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA