Dec 31, 2013

HII SASA NI FUNGA MWAKA AKAA JUU YA MNARA AKIHITAJI KUMUONA RAIS


 Wanausalama wakipanda juu ya mnara kumnusuru jamaa huyo.

 








 
Wananchi wakishuhudia tukio hilo la kufunga mwaka 2013.
 
 Jamaa huyo akiwatuhumu polisi kwa kuwabambikiza kesi wananchi wakati akiongea na wanahabari baada ya kushushwa kutoka kwenye mnara.

 Mwanaume mmoja ambaye hakufahamika jina lake mara moja amepanda juu ya mnara wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom uliopo Ubungo katika eneo la ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS)  jijini Dar es Salaam na kutaka kujirusha.

Mwanaume huyo amedai alitaka kufanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya kudai kufungwa miaka sita jela kwa kubambikiziwa kesi na  polisi.

Mwanzoni alikataa katakata kushuka kutoka katika mnara huo akidai mpaka Rais Kikwete afike eneo hilo aweze kumweleza kero yake hiyo japo wanausalama walifanikiwa kutumia mbinu zao kumshawishi ashijirushe na kufanikiwa kushuka naye.





(PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)
 

0 Weka maoni yako hapa:

Post a Comment

COMMENT HAPA